• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
SONGWE REGION
SONGWE REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa MKOA WA SONGWE

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Sehemu
      • Mipango na Uratibu
      • Idara ya Elimu
      • Huduma za Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
  • Wilaya
    • Mbozi DC
    • Songwe DC
    • Momba DC
    • Ileje DC
  • Halmashauri
    • Mbozi
    • Ileje
    • Momba
    • Songwe
    • Tunduma
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Mifugo
    • Madini
    • Kilimo
    • Biashara
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya na Ustawi Wa Jamii
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma ya Mifugo na Uvuvi
    • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
    • Mipango na Takwimu
    • Ujenzi
  • Machapisho
    • Sheria
    • Miongozo
    • Sera
    • Fomu za Maombi
    • Utaratibu
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WAZIRI WA MAJI KAMWELWE ATAHADHARISHA KUWAFUKUZA WAHANDISI

Posted on: May 23rd, 2018

 Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isaack Kamwelwe ametahadharisha kuwafukuza kazi na kuwashitaki wahandisi wa serikali wanaokosa uzalendo na kuhujumu miradi ya maji katika hatua ya usanifu na usimamizi kwa kupitisha vifaa vilivyo chini ya viwango.

Mhandisi Kamwelwe ametoa tahadhari hiyo wakati wa ziara yake Mkoani Songwe ya kukagua utekelezaji wa miradi mitatu ya maji ya Iyula na Itaka katika halmashauri ya Mbozi, mradi wa Umwagiliaji Naming’ongo katika halmashauri ya Momba na mradi wa Maji Tunduma katika halmasahuri ya Tunduma.

“Miradi mingi inakamilika na kuzinduliwa na viongozi wakubwa wa kitaifa lakini mabomba yanaanza kupasuka muda mfupi tu baada ya wananchi kuanza kupata maji kwakuwa hayana viwango, wahandisi badilikeni na hili likitokea hauna ajira na kushitakiwa juu”, amesisitiza Kamwelwe.

Ameongeza kuwa kukamilika kwa miradi ya maji hakutakuwa na tija endapo shughuli za utafiti wa vyanzo vingine imara vya maji hazitafanyika pamoja na kutunza vyanzo vya maji vilivyopo kwa ajili ya uendelevu wa miradi hiyo kwa muda mrefu.

“Hatutaki kusikia mradi unatoa maji kwa muda mfupi kisha maji yanaisha kwenye vyanzo, hivyo naagiza taasisi ya bonde la ziwa Rukwa washirikiane na taasisi nyingine pamoja na ofisi za wakuu wa wilaya kutafuta vyanzo vingine vya maji pamoja na ulinzi wa vyanzo vilivyopo”, amebainisha Mhandisi Kamwelwe.

Kwa Upande wao wananchi wameiomba serikali kuwepo kwa uwazi na ushirikishwaji katika hatua zote za ujenzi wa miradi tangu hatua ya usanifu ili kujenga uelewa juu ya miradi hiyo na kuondoa migogoro.

Ujenzi wa miradi ya maji ya Iyula, Itaka na Tunduma inatarajiwa kutoa huduma ya maji kwa wananchi takribani laki moja ambao watakuwa wanapata maji kwa umbali usiozidi mita 400 sawa na mwongozo wa sera ya maji ya mwaka 2002.

Matangazo

  • ILEJE DC WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2021 December 18, 2020
  • MBOZI DC WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2021 December 18, 2020
  • MOMBA DC WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2021 December 18, 2020
  • SONGWE DC WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2021 December 18, 2020
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Dkt. SHEKALAGHE VYUO VYA UFUNDI NA VIKUNDI VYA UJASILIAMALI MBADALA KWA WANAFUNZI AMBAO HAWAJAFAULU

    December 18, 2020
  • Dkt. SHEKALAGHE AZITAKA HALMASHAURI KUTENGA PESA YA UJENZI WA MADARASA KILA MWAKA.

    December 18, 2020
  • SONGWE: WANANCHI WAHIMIZWA KUPIMA UKIMWI KUJUA HALI ZAO KUEPUKA MAAMBUKIZI MAPYA

    December 01, 2020
  • RC MWANGELA AWATAKA WAFANYABIASHARA KUUZA BIDHAA KWA BEI ELEKEZI

    November 28, 2020
  • Angalia zote

Video

ELIMU KWA WATOTO KIPINDI CHA CORONA
Video za Ziada

Kurasa za Karibu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • SALARY SLIP PORTAL
  • AJIRA

Kurasa Mashuhuri

  • IKULU
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Boma Road, Vwawa, Mbozi

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE

    Simu: 025 2580305

    Simu ya Kiganjani: 025 2580305

    Barua pepe: ras.songwe@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.