HISTORIA.
Wabungu ni kabila ambalo linapatikana katika wilaya ya Songwe na linachukua asilimia 50 ya wakazi wa wilaya ya Songwe likifuatiwa na Wasukuma, Wanyiha na Wanyamwanga.
Inasadikika kuwa Wabungu asili yao ni Wasagara kutoka Kilosa Morogoro. Walihamia karibu na mlima Kwimba kwa ajili ya tabia yao ya uwindaji. Mpaka sasa wanafanya matambiko yao katika mlima huo.
UTATUZI WA MIGOGORO
Pamoja na serikali kupunguza nguvu ya machifu bado wanashiriki katika maswala mbalimbali kama kutatua ugomvi wa koo na koo, mauaji ya ushirikina n.k. Wabungu wanaamini kuwa makosa ya mtu mmoja yanahusisha ukoo mzima na inabidi utatuzi uwe wa ukoo mzima.
HIFADHI YA MAZINGIRA
Chifu wa sasa Mwanvungo Wangu alisema hakubaliani kabisa jinsi serikali inavyowachukulia hatua waharifu wa mazingira kwa sababu wakati wa utawala wa Kichifu mtu akiharibu mazingira alikuwa anachapwa viboko hadharani na kutozwa faini ya ng’ombe lakini sasa adhabu ni ndogo ndiyo maana mazingira yanazidi kuharibika na mvua zimepungua na hazinyeshi kwa wakati. Mwavongo aliongeza kuwa misitu ina faida ya kuwinda wanyama kwa ajili ya mboga, dawa za asili, kuleta mvua, Heshima ya Kabila, kupata kuni, miti ya ujenzi na Mbao.
SHUGHULI ZA KIUCHUMI.
Wabungu wanajishughulisha na shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kilimo, Ufugaji, Uvuvi, Uchimbaji mdogo wa Madini na Uhunzi. Katika kilimo wanalima Mahindi, Mtama, Ulezi na Jamii ya mikunde kama Kunde, Maharage n.k.; Wanafuga ng’ombe, Punda kwa usafiri, Mbuzi, Kondoo; Wananchi Wanachimba dhahabu kwa teknolojia duni. Wahunzi wanatengeneza zana za matumizi ya nyumbani kama shoka, Nyengo. Vilevile zana za kilimo kama majembe madogo ya kupandia na Silaha kama Mikuki na mishale.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.