Chifu wa Wanyamwanga Jubeck Chipanzyamakandi Mkoma wa 27 (katikati) akiwa na mke wake Lindilipanji Mkoma na msaidizi wa Chifu Aston Ernest
HISTORIA.
Iinasimuliwa kuwa Wanyamwanga walitokea nchi ya Cameron wakapitia Zaire, kutoka Zaire liliongozwa na Chifu Msyani hadi kando ya ziwa Mwelu Zambia, Isoka, Mwenzo kenye mbuga ya Mwanga (iliyozaa jina la kabila la Wanyamwanga). Eneo la utawala wa Wanyamwanga linagusa nchi mbili ya Zambia na Tanzania upande wa Magharibi mwa Wilaya ya Momba. Chifu Msyani wa Kwanza anakumbukwa na Wazambia waliompokea akitokea Zaire uwezo wake wa kuhifadhi mbegu za mazao kwenye nyele zake, uwindani mahiri na Uhunzi wake.
Kwa sasa Chifu mkuu ni Jubeck Mkoma anayetawala akiwa kwenye makao makuu yakiwa Msangano, Momba.
Wanyamwanga wanafikia asilimia 70 ya wakazi wa Wilaya ya Momba wakifuatiwa na Wanyiha, Wandali, Wasukuma na mchanganyiko wa makabila katika Mji wa Tunduma.
.
UTATUZI WA MIGOGORO
Pamoja na serikali kupunguza nguvu ya machifu bado wanashiriki katika maswala mbalimbali kama kutatua ugomvi wa koo na koo baada ya hukumu ya serikali kwa mfano kupatanisha koo baada ya kesi ya mauji, mauaji kwa njia ya ushirikina n.k Wanyamwanga wanachukulia tatizo la mtuhumiwa kuwa na ni tazizo la ukoo na kutatuliwa kiukoo wakiamini kuwa maadili ya watoto yanafanywa na ukoo hadi jamii nzima vivyo hivyo na utatuzi unatakiwa uhusishe ukoo wa mtuhumiwa au watuhumiwa.
HIFADHI YA MAZINGIRA
Wanyamwanga ni maarufu kwa kilimo cha kukata matawi ya miti, kuchoma, kulima na kupanda mazao (Ntemele). Aidha Chifu Mkoma alisema kuwa utawala wake unaheshimiwa sana upande wa Zambia ndiyo maana uharifu upande wa Zambia ni mdogo ukilinganisha na Tanzania na hata uharibifu wa kukata miti na kuchoma mkaa unafanywa na Watanzania wanaovamia misitu ya Zambia. Aliongeza kuwa misitu ina faida kwa ajili ya kufanyia matambiko, kuwinda wanyama wa porini, kupata dawa za asili, mbao, Kuni, Boriti za kujengea na kuleta mvua. Alisema pia kuwa uharibifu wa mazingira unaongezeka kutokana na wahamiaji wafugaji ambao wanaingia na ng’ombe wengi bila kufuata utaratibu na kuharibu vyanzo vya maji. Alimaliza kwa kusema robo tatu ya misitu yote inayooneka mikubwa ipo chini ya ulinzi wa Chifu kwa sababu inatumika kwa ajili ya matambiko.
SHUGHULI ZA KIUCHUMI.
Wanyamwanga ni Wakulima, Wafugaji na Wawindaji. Katika kilimo wanalima Mahindi, Mtama, Ulezi na Jamii ya mikunde kama Kunde, Maharage n.k.; Wanafuga ng’ombe, Punda kwa usafiri, Mbuzi, Kondoo, Kuku na Kanga; Wahunzi wanatengeneza zana za matumizi ya nyumbani kama shoka, Nyengo. Vilevile zana za kilimo kama majembe madogo (Mkolo) ya kupandia na Silaha kama Mikuki na mishale.
.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.