• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
SONGWE REGION
SONGWE REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa MKOA WA SONGWE

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Sehemu
      • Mipango na Uratibu
      • Idara ya Elimu
      • Huduma za Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
  • Wilaya
    • Mbozi DC
    • Songwe DC
    • Momba DC
    • Ileje DC
  • Halmashauri
    • Mbozi
    • Ileje
    • Momba
    • Songwe
    • Tunduma
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Mifugo
    • Madini
    • Kilimo
    • Biashara
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya na Ustawi Wa Jamii
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma ya Mifugo na Uvuvi
    • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
    • Mipango na Takwimu
    • Ujenzi
  • Machapisho
    • Sheria
    • Miongozo
    • Sera
    • Fomu za Maombi
    • Utaratibu
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

KILIMO

SEKTA YA KILIMO MKOA WA SONGWE

Mkoa wa Songwe una hali nzuri ya hewa na mvua za kutosha kuwezesha kuzalisha mazao ya kilimo. Mkoa unakadiriwa kuwa na jumla ya Hekta 1, 918,776.94 zinazofaa kwa kilimo, kati ya hizo jumla ya Hekta 411,575 zinalimwa mazao ya chakula na Hekta 134,343 mazao ya biashara.

Mazao makuu ya chakula yanayozalishwa Mkoa wa Songwe ni Mahindi, Mpunga, Maharage Mtama  na Karanga. Mazao mengine ni Viazi Mviringo, Viazi Vitamu, Mhogo, Njegere, Mboga na Matunda.   Mazao ya Hahindi, Mpunga na Maharage pamoja na kutumika kama mazao makuu ya chakula, ziada inayopatikana huuzwa ili kuongeza kipato cha wakulima.

Mazao makuu ya biashara yanayolimwa Mkoa wa Songwe  ni Kahawa, Tumbaku, Iliki, Pareto, Alizeti, Ufuta na Kiasi kidogo cha zao la Kokoa linalolimwa katika kijiji cha Kapeta kinachopakana na Mkoa wa Mbeya Wilaya ya Kyela.

Uzalishaji wa Mazao ya Chakula na Biashara

Mkoa wa Songwe una hali nzuri ya hewa na mvua za kutosha kuwezesha kuzalisha mazao ya kilimo. Mkoa unakadiriwa kuwa na jumla ya Hekta 1,918,776.94 zinazofaa kwa kilimo, kati ya hizo jumla ya Hekta 411,575 zinalimwa mazao ya chakula na Hekta 134,343 mazao ya biashara.

Mwaka 2016/2017  Hekta 411,575 zililimwa mazao ya chakula na  kuvunwa tani 995,051 hadi kufikia Juni 2017, sawa na  92% ya lengo la Mwaka la tani 1,070,457. Mahitaji ya chakula katika Mkoa inakadiriwa kufikia tani 467,355, hivyo kuwa na ziada ya tani 527,696.

 Mchanganuo wa utekelezaji wa malengo ya uzalishaji msimu wa 2016/2017 umeoneshwa kwenye Jedwali

Jedwali: Uzalishaji wa Mazao ya Chakula na Biashara hadi Juni, 2017

Halmashauri

Malengo ya Mazao ya Chakula

Utekelezaji wa Mazao ya Chakula

Malengo ya Mazao ya Biashara

Utekelezaji wa Mazao ya Biashara

Eneo (Ha)

Uzalishaji (Tani)

Eneo (Ha)

Uzalishaji (Tani)

Eneo (Ha)

Uzalishaji (Tani)

Eneo (Ha)

Uzalishaji (Tani)

Ileje

80,110

384,831

81,210

489,651

10,396

6,936

10,204

6,760

Songwe

42,929.00

106,469.00

31,197.21

59,917.47

34,280.00

59,889.70

14,435.02

12,232.21

Mbozi

184,160

391,715

112,746

336,757

67,679

43,813

67,679

38,117

Momba

92,219

166,222

67,984

98,152

19,590

23,794

19,590

18,338

Tunduma TC

12,157.16

21,220

6,246

10,574

2,398

1,561

1,762

1,102

JUMLA 

   411,575

  1,070,457

   299,383

    995,051

   134,343

    135,994

   113,670

      76,549

Chanzo: Halmashauri za Wilaya, na Mji wa Tunduma 2017

 

Jedwali: Wastani wa bei za mazao sokoni kufikia 15 Desemba, 2017

Na
Aina ya Chakula
Upatikanaji wa
Chakula Sokoni
Bei ya chini
kwa kilo
Bei ya juu
kwa kilo
Wastani wa bei
Kwa kilo
1
Mahindi
Kinapatikana
278
361
320
2
Mchele
Kinapatikana
1900
2200
2050
4
Ulezi
Kinapatikana
800
1000
900
6
Viazi vitamu
Kinapatikana
500
600
550
7
Maharage
Kinapatikana
1,500
2000
1750
8
Mikunde mingine
Kinapatikana
1,500
1,800
1650
9
Mtama
Kinapatikana
400
600
500
10
Soya
Kinapatikana
800
1000
900
11
Alizeti
Kinapatikana
350
500
425
12
Ngano
Kinapatikana
1,100
1,600
1,350
13
Karanga
Kinapatikana
1,500
2,000
1,750
14
Viazi mviringo
Kinapatikana
800
1,150
950


Chanzo: Halmashauri za Wilaya na Mji Tunduma 2017

 

MALENGO YA UZALISHAJI MSIMU 2017/2018.

Malengo ya Uzalishaji Mazao ya Chakula na Biashara 2017/2018.

Malengo ya Mkoa kwa msimu wa mwaka 2017/2018 ni kuzalisha tani 1,276,836 za mazao ya chakula na tani 136,650 za mazao ya biashara. Hali ya hewa msimu huu ni nzuri   na mvua zilianza kunyesha wiki ya kwanza mwezi Novemba, 2017. Hali ya mazao kwa ujumla ni nzuri na wananchi wanaendelea na shughuli ya kupanda mazao ya chakula mpaka kufikia traehe 15 zaidi ya 75% ya wakulima wameshapanda na walio salia mpaka kufikia tarehe 15/01/2018 watakuwa wamekamilisha.

Mchanganuo wa malengo ya uzalishaji wa mazao umeainishwa katika Jedwali

Jedwali :Malengo ya uzalishaji wa Mazao ya Chakula na Biashara msimu 2017/2018

HALMASHAURI

Mazao ya Chakula 

Mazao ya Biashara

Eneo (Ha)

Mavuno (Tani)

Eneo (Ha)

Mavuno (Tani)

Ileje

81,054

532,694

10,396

6,936

Songwe

46,981

94,309

34,245

59,856

Mbozi

186,189

461,254

67,679

43,813

Momba

92,486

171,123

19,590

23,794

Tunduma TC

12,425

17,457

2,502

2,251

JUMLA

419,135

1,276,836

134,412

136,650

Chanzo: Halmashauri za Wilaya na Mji Tunduma 2017   

 

PEMBEJEO ZA KILIMO.

  

Mahitaji ya Pembejeo msimu 2017/2018.

Mkoa wa Songwe katika msimu 2017/2018 umepanga kutumia pembejeo za kilimo kwa upande wa mbolea za kupandia  tani  43,625,  kukuzia tani 62,953  na mbegu bora tani 5,772 ili kutekeleza malengo ya uzalishaji ya tani 1,276,836 za mazao ya chakula na tani 136,650 za mazao ya biashara.

Jedwali Na. 9  likionesha mahitaji ya pembejeo kwa kila Halmashauri.

AINA YA PEMBEJEO (TANI)

 MAHITAJI (TANI/LITA) TOKA KILA WILAYA







MBOLEA YA KUPANDIA
 ILEJE (1) 
 TUNDUMA TC (2) 
 MBOZI (3) 
 MOMBA (4) 
 SONGWE (5) 
 TANI/LTS 
DAP

            6,951

      1,000

        16,315

7450

                                3,734

          35,450

NPK 20:10:10

               104

0  

          2,022

               0  

0

            2,126

NPK 10:18:20

               255

0  

          1,100

2650

                         244

            4,249

NPK 17:17:17

0

0

         1,800

0

0

            1,800

MINJINGU MAZAO

0

0

0

0

0

0

JUMLA NDOGO MBOLEA KUPANDIA

7,310

1,000

21,237

10100

3,978

43,625

MBOLEA YA KUKUZIA

 

 

 

 

 

 

UREA

            6,473

      1,950

        19,565

6,445

                                3,834

          38,267

CAN

            2,313

      1,300

          8,109

6,445

                           98

          18,265

SA

            1,484

         650

          1,587

2,700


            6,421

JUMLA NDOGO YA MBOLEA KUKUZIA

10,270

3,900

29,261

15,590

3,932

62,953

JUMLA KUU MBOLEA

17,580

4,900

50,498

25690

244

106,578

JUMLA KUU MBEGU BORA 

                1,205 

 380 

        2,640 

                  471 

                              1,076 

        5,772 

Bei elekezi ya mbolea ya kupandia na kukuzia iliyotolewa na TFRA kwa Mkoa wa Songwe ni kama inavyoonesha katika jedwali Na. 10 kwa kila Wilaya.


Jedwali likionesha bei elekezi kwa Wilaya

Na
Halmashauri
Bei elekezi ya mbolea ya kupandia -  DAP (TZS)
Bei elekezi ya mbolea ya kukuzia - Urea (TZS)
1
Ileje
54,179
41,600
2
Mbozi
54,014
41,435
3
Momba
54,300
41,721
4
Songwe
54,118
41,539
5
Tunduma
54,360
41,781

Wenyeviti wa kamati za Pembejeo Wilaya wameshauriwa kuhakikisha pembejeo zinawafikia wakulima kwa kila kata/kijiji iliwakulima waweze kupata huduma ya pembejeo kwa urahisi kwa kufuata bei elekezi ya Pembejeo iliyowekwa na Serikali, ikibidi Halmashauri zinunue pembejeo  na kuwafikishai wakulima katika maeneo yao kama hakuna wakala eneo hilo.


USAMBAZAJI  WA PEMBEJEO MSIMU 2017/2018.

Kupitia Mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja na bei elekezi ilitolewa na Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa mbolea Nchini (TFRA), bei hiyo inazingatiwa kwa kuhakikisha inamfikia mkulima ndani ya Mkoa kama ilivyo pendekezwa na TFRA. Makampuni na mawakala wa pembejeo ndani ya Mkoa wameweza kufikisha mbolea katika vituo vikubwa vya Vwawa na Mlowo ambao ni Export Traders, STACO, Yara Tanzania na Unyiha Associate ndipo mawakala wadogo hununua na kuzifikisha vijijini. Changamoto kubwa iliyopo ni malalamiko toka kwa mawakala wadogo ambao wanadai kutopata faida kutokana na gharama kuwa kubwa zinazohusisha  usafirishaji.  Kama inavyoonesha katika Jedwali namba 11 hapa chini:-

Jedwali makadirio ya gharama halisi za usambazaji mbolea

Kutoka
Kwenda
Gharama ya kusafirisha 50Kg Tsh
Bei ya jumla vwawa
Bei ya jumla pamoja na gharama za usafirishaji
Bei elekezi  ya mbolea kila Wilaya
 
Faida/Hasara
Mbozi
(Vwawa)
DAP
UREA
DAP
UREA
DAP
UREA
DAP
UREA
Ileje
1,650
52,500
40,000
54,150
41,650
54,179
41,600
29
(50)
Momba
2,400
52,500
40,000
54,900
42,400
54,300
41,721
(600)
(679)
Tunduma
1,650
52,500
40,000
54,150
41,650
54,360
41,781
210
68
Mbozi
1000
52,500
40,000
53,500
41,000
54,014
41,435
510
435
Mbeya
Songwe
1500
52,500
40,000
54,500
41,500
54,118
41,539
(382)
(39)

Kwa mchanganuo huo hapo juu baadhi ya mawakala wadogo wameshindwa kufikisha pembejeo katika wilaya na kata kutokana na kutopata tija yeyote katika biashara hiyo ukilinganisha na gharama za uendeshaji. Mh. Waziri wa Kilimo Dr. Charles J. Tizeba alitolea ufafanuzi kuwa mbolea ya awamu ya pili itakayoingia mwezi Desemba itatoa mchanganuo wa bei ya jumla na rejereja kwa wakala mkubwa ngazi ya Mkoa na Wilaya  pamoja na mgawanyo wa 12% ili mawakala wadogo waweze kufikisha pembejeo vijijini bila shida yeyote tofauti na ilivyo sasa.


KIASI CHA MBOLEA SAMBAZWA.

Kiasi cha mbolea kilicho wasilishwa ndani ya Mkoa kupitia makampuni na mawakala wakubwa pamoja na kiasi kilichokwisha sambazwa kwa wakulima tangu utaratibu huu wa uagizaji wa mbolea wa pamoja ni kama inavyo onesha katika jedwali  namba 12 hapa chini:-

Jedwali  namba 12 usambazaji wa mbolea na mawakala wa kati

Na
Jina la kampuni/ Wakala
Kiasi cha mbolea ingizwa Mkoani (Tani)
Kiasi cha Mbolea Sambazwa kwa Wakulima (Tani)
Asilimia ya usambazaji 
1
Export Traders
19,200
17,264

90%

2
STACO
629
577.6

92%

3
Unyiha Associates
1000
950

95%

4
Yara Tanzania
9,600
8,932.30

93%

5
Mawakala wa kati
5,450
4,128.60

75%

JUMLA
35,879
31,852.5

88%


UNUNUZI WA NAFAKA KUPITIA WAKALA WA TAIFA WA HIFADHI YA CHAKULA

Mwaka 2017/2018 lengo la NFRA lilikuwa kununua tani 6,000 za mahindi  kwa Nyanda za Juu Kusini, katika Mkoa wa Songwe, hadi mwisho wa msimu jumla ya tani 5,487.317 zilinunuliwa katika vituo vya Mkoa wa Songwe.

Jedwali  Ununuzi wa mahindi katika msimu 2017/2018 Mkoani Songwe

Na

Halmashauri/Kituo

Tani

1

Ileje

638.589

2

Mbozi

1,860.753

3

Momba

811.290

4

Songwe

157.270

5

Tunduma

2,019.415

Jumla

5,487.317

Chanzo: Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya ya Chakula (NFRA) 2017  

 

 KILIMO CHA UMWAGILIAJI

Katika Mkoa wa Songwe eneo linalofaa kwa kilimo cha  umwagiliaji ni 18,664.9 Ha, zilizoendelezwa ni 4,881 Ha na zinazomwagiliwa kwa njia ya asili ni 2,142 Ha, hivyo kufanya eneo la  7,023 Ha zinazomwagiliwa.

Katika mwaka 2017/2018 Mkoa unaendelea kutekeleza miradi ya kilimo katika Halmashauri zote kupitia DADPs, mapato ya ndani na wadau wengine wa maendeleo. Fedha ambazo zilipokelewa mwaka wa Fedha 2016/17 ni Jumla ya Tsh Milioni 730 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji kupitia mpango wa kuendeleza skimu ndogo ndogo za umwagiliaji nchini (SSIDP – JICA).

Aidha, fedha hizo kiasi cha Tsh. Milioni 730 zimeweza kutekeleza miradi 3 ya umwagiliaji 1) Ileje skimu ya umwagiliaji ya Sasenga kwa kusakafia mfereji mkuu mita 777.5 na kuinua urefu wa banio cm 30 ujenzi umekamilika. 2). Mbozi skimu ya umwagiliaji Mbulu mlowo ujenzi wa Gabions na tuta urefu wa 150m kwa ajili ya kuzuia maji pamoja na kufukia korongo mita za ujazo 1,200, ujenzi umekamilika 3).   Momba Skimu ya umwagiliaji Naming’ongo uchimbaji wa mfereji mkuu mita 2,560 na kusakafia urefu wa mita 800 ujenzi umekamilika.

Katika mwaka wa fedha 2017/2018 jumla ya Tsh. 622,500,000 zitatumika kuboresha miundombinu ya umwagiliaji katika Halmashauri zetu kupitia Mpango wa kuendeleza skimu ndogondogo Nchini (SSIDP – JICA)

 

Huduma za Ugani 

Sekretarieti ya Mkoa wa Songwe pamoja na Halmashauri zake 5 inahitaji Maafisa Ugani 575 Ili waweze kutoa huduma bora za ugani kwa wakulima. Mkoa unajumla ya Watumishi wa Ugani 286, upungufu ni watumishi 289. Katika fani ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika. Jedwali namba 14 hapa chini linaonesha mahitaji ya watumishi katika Mkoa wa Songwe.

Jedwali  Hali ya watumishi Mkoa wa Songwe

Na
Jina la ofisi 
Mahitaji ya watumishi 
Watumishi waliopo 
Upungufu
  •  
Sekretarieti ya Mkoa

19

5

14

  •  
Halmashauri ya Mbozi

213

117

96

  •  
Halmashauri ya Momba

132

77

55

  •  
Halmashauri ya Ileje

94

37

57

  •  
H/Mji wa  Tunduma

44

23

21

  •  
Halmashauri ya Songwe        

73

27

46

  •  
Jumla 

575

286

289

Chanzo: Halmashauri za Wilaya, na Mji wa Tunduma 2017

Ili kukabiliana na upungufu huu Mkoa kupitia Halmashauri zake unaendelea kuomba vibali vya ajira mpya kila mwaka, katika bajeti ya mwaka 2017/2018 jumla ya watumishi 157 Wanatarajiwa kuajiriwa. Aidha huduma za ugani zinatolewa kwa wakulima kwa kushirikiana na sekta binafsi/wadau wa kilimo waliopo ndani ya Mkoa wetu. 


ZANA ZA KILIMO

Mkoa umepiga hatua katika matumizi ya zana za kilimo ambapo matrekta makubwa yapo 142, matrekta madogo 110, plau 125,753, mikokoteni 108,012 majembe ya kupalilia 78, rippers 42, majembe ya kupandia 18 na maksai 137,011 Hamasa na elimu ya matumizi ya zana bora za kilimo inaendelea kutolewa ili kurahisisha shuguli za kilimo na kuongeza uzalishaji wenye tija.

  •  Jedwali: Mchanganuo wa matumizi ya zana za kilimo.


Matrekta
makubwa
Matrekta
Madogo
Plau
Mikokoteni
Majembe
kupalilia
Rippers
Majembe
Kupandia
Maksai

142

110

125,753

108,012

78

42

18

137,011


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI January 30, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • SERIKALI YA SAINI MRADI WA ZAIDI YA BILIONI 119.9 UJENZI WA MRADI WA MAJI TUNDUMA VWAWA

    March 20, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA ILEJE MHE. FARIDA MGOMI KWA NIABA YA MKUU WA MKOA AFUNGUA HUDUMA YA WIKI YA SHERIA MKOANI SONGWE

    January 25, 2025
  • TASAF MKOA WA SONGWE IMEFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI NA KUJIONEA UTOAJI WA HUDUMA KWA WANUFAIKA WA TASAF MOMBA

    January 03, 2025
  • KIKAO CHA TATHMINI YA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI NA MTOTO MKOANI SONGWE.

    November 07, 2024
  • Angalia zote

Video

ELIMU KWA WATOTO KIPINDI CHA CORONA
Video za Ziada

Kurasa za Karibu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • SALARY SLIP PORTAL
  • AJIRA

Kurasa Mashuhuri

  • IKULU
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE

    Simu: 025 2580305

    Simu ya Kiganjani: 025 2580305

    Barua pepe: ras@songwe.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.