BILIONI 20.9 KUBORESHA BARABARA, MADARAJA
Na. Nicholas Ndabila
SONGWE: Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) katika bajeti ya 2022/2023 imetenga fedha Bilioni 20.9 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Barabara yenye urefu wa Kilomita 3341.1 pamoja na madaraja.
Hayo yamesemwa na Meneja wa TARURA Mkoa wa Songwe Eng. Kilian Daudi Haule Katika hafla ya utiaji saini mikataba mitano kati ya TARURA na Makandarasi iliyosainiwa Septemba 9 na kushuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe pamoja na wakuu wa Wilaya katika ukumbi wa Mkoani.
Kampuni zilizo saini mikataba hiyo ni Kampuni ya Lusubilo Wandarasi iliyo saini mkataba waenye thamani ya Shilingi Million 56.3, HANSAF Company Limited iliyoko wilayani Ileje Mkataba wenye thamani ya Shilingi Millioni 210.1, DAR Form company Limited iliyoko wilaya Mbozi mkataba wenye thamani ya shilingi Millioni 312.37, Rwechotes Company Limited inayopatikana halmashauri ya Tunduma imesaini mkataba wenye thamani ya Shilingi Millioni 168.5 pamoja na kampuni ya GNMS Contructors Company Limited iliyoko wilaya ya Songwe iliyo saini mkataba wenye thamani ya shilingi Million 598.878.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Waziri Kindanba ameishukuru sana Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali wananchi kupitia kutekeleza miradi mbali mbali ndani na nje ya mkoa wa Songwe.
Amewataka wakandarasi kutekeleza wajibu wao na kuwa waadirifu kufanya kazi bora na kukamilisha miradi hiyo kwa wakati lakini pia amewasihi Uongozi wa TARURA wilaya na Mkoa kusimamia miradi hiyo kwa ukaribu na ubora kutokana na masharti ya mikataba iliyo sainiwa.
"Kama jambo hulifuatilii na kulisimamia kwa ukaribu litafanywa chini ya kiwango lazima ukague lazima uende eneo la kazi uangalie nini kinafanyika" Mhe. Waziri Kindamba Mkuu wa Mkoa wa Songwe.
Mwenyekiti CCM Mkoa wa Songwe Ndug. Elynico Mkola amemshukuru Rais wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza Ilani Chama Cha Mapinduzi kwa vitendo kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya huduma za afya na jamii.
Fungo Atukuzwe Alex mkandarasi wa kampuni ya HANSAF CO. Limited inayo patikana Wilaya ya Ileje ameishukuru Serikali kwa kuwaamini na kuahidi kuitekeleza miradi kwa wakati na kwa weledi kwa hali ya juu kama walivyo ingia makubaliano na Serikali katika mkataba uliosainiwa.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.