Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dkt. Francis Michael, na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara, katika kushughulikia changamoto za usafirishaji wa mizigo katika kituo cha forodha katika mpaka wa Tunduma. Mpaka huu unaunganisha Tanzania na nchi jirani kama Zambia, Zimbabwe, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na ni njia muhimu ya usafirishaji wa mizigo katika eneo hilo.
Mhe. Dkt. Francis Michael, ameipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kuchukua hatua za kuongeza nguvu katika kutatua changamoto za usafirishaji katika eneo hilo. Ameona maboresho haya yatakuwa na athari chanya kwa maendeleo ya mkoa wa Songwe na pia kuchangia katika miradi mingine ya upanuzi wa barabara, kama vile Barabara ya TANZAM.
Prof. Kahyarara amesema kuwa Serikali imechukua hatua za haraka kushughulikia changamoto hizo, ikiwa ni pamoja na kusimika mashine za ukaguzi wa mizigo na kuboresha mifumo ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) katika mpaka huo. Lengo kuu ni kurahisisha usafirishaji wa mizigo, kupunguza muda wa ukaguzi, na kuimarisha huduma zinazotolewa katika eneo hilo.
Prof. Kahyarara pia ameeleza kuwa maboresho haya yataleta faida kadhaa, ikiwa ni pamoja na kupunguza muda wa magari yanayopita mpakani, kuboresha ufanisi katika Bandari ya Dar es Salaam, kupunguza bei za bidhaa zinazosafirishwa kupitia barabara, na kwa ujumla, kuboresha usafirishaji na biashara kati ya nchi jirani.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Songwe, SSP. Joseph Bukombe, ameeleza kuwa Jeshi la Polisi limejiwekea utaratibu maalum wa kusaidia kusimamia utaratibu wa foleni ili kupunguza msongamano wa magari, hususan kwa watumiaji wa barabara wanaokwenda mikoa ya Rukwa, Katavi, na Kigoma kupitia mkoa wa Songwe.
Hatua hizi za Serikali zinaweza kusaidia kuboresha biashara na usafirishaji katika eneo hilo, kuchangia ukuaji wa uchumi, na kuimarisha huduma za usafirishaji katika mpaka wa Tunduma.
Sehemu ya Viongozi wa taasisi za Serikali na Wadau wa Usafirishaji wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Dkt. Francis Michael (hayupoo pichani) wakati Mkuu huyo alipokutana na Prof. Kahyarara Mkoani Songwe, mwishoni mwa wiki.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.