CHANJO YA UVIKO-19 OFISI KWA OFISI, NYUMBA KWA NYUMBA
Na. Nicholas Ndabila
SONGWE: Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakipata chanjo ya UVIKO-19 ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya chanjo ya UVIKO-19 ya ofisi kwa ofisi, Nyumba kwa nyumba.
Watalamu wa Afya wanaendelea na Kampeni ya chanjo ya UVIKO-19 Nyumba kwa nyumba kwa mkoa mzima na sasa tunaanza ofisi kwa ofisi, amesema Dkt. Rose Alfred.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Waziri Kindamba amesema kampeni hii itakwenda sambamba na ofisi kwa ofisi ili kuwafikia watu wengi na kuwakinga na ugonjwa wa wa UVIKO-19 ambao bado upo.
"Kwa sasa Mkoa wa Songwe una asilimia 17 tu za watu waliopata chanjo na kufanya Mkoa uwe mwisho kitaifa" Mhe. Waziri Kindamba.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dkt. Rose Alfredy amesema watalamu watapita kila ofisi iliyopo mkoani, pamoja na mikusanyiko mbalimbali lengo ni kufkia asilimia 70 ifikapo Disemba 2022 ya watu wote wenye umri wa zaidi ya miaka 18 wawe wamepata chanjo ya UVIKO-19.
Tumebaini watu wengi wanahitaji chanjo ila wanaona uvivu na wanakosa muda wa kwenda Kituo cha huduma za Afya kupata chanjo, sasa tunawafuta uko waliko, amesema Dkt. Rose Alfredy.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.