Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt Francis Michael ameongoza Warsha elekekezi ya Dira ya Taifa ya maendeleo 2050 iliofanyika katika Mkoa wa Songwe.
Warsha hii iliyokusanya viongozi wa ngazi mbalimbali na wadau wa maendeleo, ililenga kuweka msingi imara wa maendeleo ya kitaifa kwa miongo ijayo.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, alisisitiza umuhimu wa kujenga mustakabali wa Taifa kwa kuzingatia mabadiliko ya kijamii, kiuchumi, na kisiasa. Alieleza kuwa malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ni kuongeza ufanisi wa utendaji katika kila sekta na kuhakikisha maendeleo endelevu yanapatikana kwa wananchi wote.
Warsha hii ilikuwa jukwaa muhimu ambapo washiriki walishirikiana mawazo na kujadiliana njia bora za kufikia malengo yaliyowekwa. Masuala kama maendeleo ya miundombinu, elimu, afya, kilimo, viwanda, na uhifadhi wa mazingira vilipewa kipaumbele katika majadiliano.
Dkt Francis aliwahimiza washiriki kufanya kazi kwa ushirikiano na kuweka mbele maslahi ya Taifa. Alisisitiza kuwa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 unahitaji juhudi za pamoja kutoka kwa kila mmoja ili kufikia mafanikio yanayotarajiwa.
Washiriki wa warsha walipokea kwa mikono miwili mwelekeo wa kujenga Taifa bora na lenye mafanikio endelevu ifikapo mwaka 2050. Waliishukuru serikali ya Mkoa wa Songwe chini ya uongozi wa Mkuu wa Mkoa, Dkt. Francis Michael, kwa kuandaa warsha hii muhimu ambayo imechagiza ari ya kufanikisha malengo ya maendeleo ya Taifa.
Akifunga Warsha hiyo Elekekezi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Dkt. Francis Michael aliahidi kusimamia utekelezaji wa mipango na mikakati iliyowekwa kwa dhati na kuhakikisha kwamba maendeleo yanawafikia wananchi wa Mkoa wa Songwe na Tanzania kwa ujumla.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.