DKT. KASULULU AZITAKA CHMT ZIFANYE KAZI KWA KUFUATA MIONGOZO, SERA NA SHERIA ZA AFYA.MBOZI: Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dkt. Boniface Kasululu amezitaka Timu za usimamizi na uendeshaji wa huduma za Afya ngazi Halmashauri kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, miongozo na sera ambazo zimetolewa na Serikali na Wizara ya sekta ya Afya.Dkt. Kasululu amesema hayo wakati akiongea na Timu ya usimamizi na uendeshaji wa huduma za Afya (CHMT) ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, 7 Mei 2022.'Kama wewe ni mratibu wa chanjo basi lazima ufanye kazi kwa kufuata miongozo ya chanzo na ujue kila chanjo kwa kina na kama wewe ni Ustawi wa jamii basi lazima uzijui sheria zote, miongozo na kanunni za Ustawi wa jamii" Dkt. Boniface Kasululu.Pia, Dkt. Kasululu amemtaka kila mjumbe wa CHMT awe na miongozo na kuisoma vizuri ili azifahamu vizuri sheria mbalimbali za Afya kwa ajili ya kumsaidia katika utendaji kazi wake.Mganga Mkuu wa Mkoa anaendelea na utaratibu wa kukutana na watalamu wa Afya kuanzia ngazi ya Halmashauri hadi kwenye vituo vya kutolea huduma kwa lengo la kuwakumbusha misingi na kanunni za sekta ya Afya katika kuwahudumia wananchi wa Mkoa wa Songwe.MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.