SONGWE: RAS SHEKALAGHE: KUTATUA CHANGAMOTO ZILIZOPO HOSPITALI TEULE NA HOSPITALI MPYA YA MKOA ITAKAPOANZA.
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Dr. Self Shekalaghe ameuagiza uongozi wa Hospitali Teule ya Mkoa wa Songwe kumuletea changamoto zote zinazowakabili katika utendaji kazi zilizopo sasa na zile ambazo wanaona zitatokea pale watakapoamia kwenye Hospitali mpya ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe.
“Nataka mukiamia kwenye Hospitali mpya ya Rufaa ya Mkoa changamoto zilizopo hapa zisijirudie na zile ambazo munaona zitajitokeza basi tuone jinsi gani ya kuzimaliza haraka kabla hamjaamia pamoja na kuzitatua zilizopo kwenye Hospitali Teule hii” Katibu Tawala mkoa wa Songwe, Dr. Self Shekalaghe akiongea na watumishi wa Hospitali Teule ya Mkoa wa Songwe, 16 Novemba 2020.
Pia, Katibu Tawala wa Mkoa ameagiza ifikapo 23 Novemba 2020 kuanza kwa ujenzi wa eneo la kusubiria wagonjwa katika Hospitali Teule ya Mkoa wa Songwe ambayo imekuwa ni kero kwa watu wanaokuja kuona au kuleta wagonjwa.
Wakati huhuo Dr. Shekalaghe ametaka kupata tathimini ya fedha ya kila mwezi kuanzia Januari-June 2020 na kwa mwaka wa fedha 2020/2021 hadi sasa ikionyesha kila Idara kwenye Hospitali ilichopata kwa mwezi, lengo ilikuwa ipate ngapi na kipi Serikali imepeleka pamoja na kilichorudi.
Mkoa wa Songwe unatumia Hospitali iliyokuwa ya Wilaya ya Mbozi ambayo kwa sasa inaitwa Hospitali Teule ya Mkoa wa Songwe na kwa sasa Mkoa wa Songwe unajenga Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ambayo iko hatua za ukamilishaji.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.