• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
SONGWE REGION
SONGWE REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa MKOA WA SONGWE

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Sehemu
      • Mipango na Uratibu
      • Idara ya Elimu
      • Huduma za Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
  • Wilaya
    • Mbozi DC
    • Songwe DC
    • Momba DC
    • Ileje DC
  • Halmashauri
    • Mbozi
    • Ileje
    • Momba
    • Songwe
    • Tunduma
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Mifugo
    • Madini
    • Kilimo
    • Biashara
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya na Ustawi Wa Jamii
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma ya Mifugo na Uvuvi
    • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
    • Mipango na Takwimu
    • Ujenzi
  • Machapisho
    • Sheria
    • Miongozo
    • Sera
    • Fomu za Maombi
    • Utaratibu
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

ELIMU JUU YA TAHADHARI YA CORONA BADO HAITOSHELEZI

Posted on: April 3rd, 2020

Mpaka sasa hakuna dawa wala chanjo ya Ugonjwa wa Virusi vya Corona hivyo njia bora ya kupambana na ugonjwa huo ni utoaji wa elimu juu ya tahadhari za kujikinga ili mtu asipate ugonjwa huo ambapo kwa Mkoa wa Songwe Elimu hiyo bado haitoshelezi.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela ameyasema hayo wakati wa kikao cha Wadau wa Afya waliokutana mapema leo kujadili utayari wa kukabiliana na Ugonjwa wa Virusi vya Corona kwa Mkoa wa Songwe.

Brig. Jen. Mwangela amesema hadi sasa kuna maeneo bado wananchi hawajapata elimu ya tahadhari ya kujikinga na virusi vya Corona huku akiwaagiza Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Waganga Wakuu wa Wilaya zote kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi wote.

Amesema elimu itolewe kwa kutumia vyombo vyote vya habari vilivyopo na kwa namna zote bora ambazo zitawezesha kuwafikia wananchi wote na kwa wataalamu wa afya ambao baadhi yao bado  hawana elimu hiyo.

Brig. Jen. Mwangela ameongeza kwa kulitaka Jeshi la Polisi Mkoani Songwe kuendelea kufanya ukaguzi katika mabasi yote endapo yanazingatia tahadhari za kujikinga na Ugonjwa wa Virusi vya Corona pia wananchi wote waepuke mikusanyiko isiyo ya lazima.

Amesema taasisi zote ziendelee kuchukua hatua za tahadhari zilizo elekezwa na wataalamu wa Afya huku akimtaka Mganga Mkuu wa Mkoa kuchukua hatua za haraka kutokana na kuwa maji ya kunawa katika geti la kuingilia Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa yalikua hayana dawa hali ambayo sio sahihi.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt Hamad Nyembea amesema atahakikisha tahadhari za kujikinga na Ugonjwa wa Virusi vya Corona zinachukuliwa katika hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe huku akieleza kuwa tayari wameweka utaratibu wa kupima jotoridi watu wote wanaoingia hospitalini hapo.

Dkt Nyembea amesema hapo awali watu wengi walikua wakichukua tahadhari  juu ya ugonjwa wa Virusi vya Corona na Kufuata maelekezo ya wataalamu wa Afya lakini sasa baadhi wameanza kupuuzia hivyo anawasihi wasifanye hivyo kwani ugonjwa huo bado ni tishio.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila amesema Mkoa wa Songwe ni lango kuu la kuingilia na kutoka katika nchi za SADC hivyo hatua za tahadhari  juu ya Corona zinazo chukuliwa zinapaswa kuwa madhubuti Zaidi kuliko maeneo mengine.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI January 30, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • RC CHONGOLO AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI WILAYA YA MOMBA KUJADILI HOJA ZA CAG

    June 11, 2025
  • RC CHONGOLO AONGOZA KIKAO CHA KUJADILI HOJA ZILIZO BAINISHWA KATIKA RIPOTI YA CAG HALMASHAURI YA MBOZI

    June 10, 2025
  • RC CHONGOLO APIONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA ILEJE KWA KUPATA HATI SAFI

    June 10, 2025
  • SERIKALI YA SAINI MRADI WA ZAIDI YA BILIONI 119.9 UJENZI WA MRADI WA MAJI TUNDUMA VWAWA

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

ELIMU KWA WATOTO KIPINDI CHA CORONA
Video za Ziada

Kurasa za Karibu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • SALARY SLIP PORTAL
  • AJIRA

Kurasa Mashuhuri

  • IKULU
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE

    Simu: 025 2580305

    Simu ya Kiganjani: 025 2580305

    Barua pepe: ras@songwe.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.