FANYA KAZI NENDA LIKIZO, RAS SENEDA.
SONGWE: Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Bi. Happiness Seneda ametoa wito kwa watumishi kuchukua likizo muda unapofika.
Katibu Tawala Mkoa amesema ili mtumishi aweze kufanya kazi kwa ufanisi kazini likizo ni ya lazima ni muhimu.
Katibu Tawala amesma hayo wakati akiongea na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi na Halmashauri ya Mji Tunduma kwa nyakati tofauti Agosti 10 alipofanya ziara maalumu ya kujitambulisha kwako.
"Ndugu zangu kazi izi tunafanya ni ngumu sana, hivyo lazima mtumishi upate muda wa kupumzika muda wako unapokuwa umefika" Bi. Happiness Seneda
Pia, Katibu Tawala Mkoa wa Songwe amewataka wakuu wa Idara na vitengo kuwashirikisha kazi zote watumishi walio chini yao ili mtumishi anapokwenda likizo basi kuwe na mtu wa kufanya kazi izo.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.