FOODtech NA MIKAKATI YA KUJENGA KIWANDA CHA MBOLEA SONGWE.SONGWE:
Kampuni ya FOODtech kutoka nchini Zimbabwe imekuja Songwe kuangalia uwezekano wa kujenga kiwanda cha Mbolea na kuzalisha Mbolea ya asili ambayo inatokana na masalia ya makaa ya mawe katika Mgodi wa Kiwila uliopo Wilaya ya Ileje.Mtendaji Mkuu wa FOODtech, Ngoni Chandiwana amesema wamevutiwa kuja kuwekeza Songwe kwa sababu ya uwepo wa malighafi ya kuzalisha Mbolea, miundombinu ya reli ya TAZARA na lengo la FOODtech ni kushika soko la Afrika Mashariki."Mazungumzo yakienda vizuri na Serikali ya Tanzania tunaanza kuwekeza muda wowote kuanzia sasa kwani mahitaji ya Mbolea ni makubwa na sisi tumeamua kutumia maligahafi za Afrika kuzalisha Mbolea ili kupunguza bei ya Mbolea kwenye soko" Mtendaji Mkuu wa FOODtech, Ngoni Chandiwana.Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amesema Songwe ndio Mkoa ambao unaongoza kwa matumizi ya Mbolea hivyo kitendo cha FOODtech kuonyesha nia ya kujenga kiwanda hapa Songwe wamepatia.Mhe. Omary Mgumba amesema ujio wa FOODtech unakwenda kuongeza upana wa matumizi ya makaa ya mawe, kuongeza ajira kwa watanzania, kuongeza ukuwaji wa uchumi wa Mkoa wa Songwe.Pia, Mkuu wa Mkoa amesema hadi sasa Mgodi wa Kiwila una akiba ya tani Milioni 110 ambazo bado hazijachimbwa za makaa ya mawe, tani Milioni 98 zipo katika machimbo ya Kabulo na tani Milioni 12 zipo katika Mgodi wa chini wa Kiwila.Aidha, Mkuu wa Mkoa, Mhe. Omary Mgumba amesema hadi sasa Nchi ya Nigeria imeanza kununua tani laki 702,000, uku mazungumzo kati ya Nchi ya China kununua tani Milioni 1.2 na India kununua tani laki 6 yakiendelea.Uwekezaji wa FOODtech unatarajia kuzalisha Mbolea zaidi ya tani 200,000 kwa mwaka.MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.