HALMASHAURI YA SONGWE JITATHIMINI KWA KUPATA HATI YA MASHAKA: RC MICHAEL.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Dkt. Francis Michael ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe kujitathimini na kujipanga vizuri na kutoruhusu tena Halmashauri hiyo kupata hati ya mashaka kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Mkuu wa Mkoa ametoa agizo hilo kwenye Baraza la kujadili Hoja za Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) lililofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Songwe.
"Ninafahanu uwezo wwenu ilivyo vizuri, sina shaka kabisa na Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi pamoja na Baraza la Madiwani jipangeni vizuri" Mhe. Dkt. Francis Michael.
Mhe. Dkt. Francis Michael amelitaka Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Songwe kusimamia kwa ukaribu Halmashauri yao ili wasipate tena hati ya mashaka kwa mwaka fedha 2022/2023.
"Waheshimiwa madiwani tunapokuwa tuna hoja nyingi kwenye Halmashauri na kupata hati ya mashaka hii ina maanisha kwamba Madiwani hamsimamimi Halmashauri, sasa msikubali watalamu wenu wawafanye kuwa nyie hamjui kitu chukueni hatua" Mhe. Dkt. Francis Michael.
Mkaguzi wa nje wa Mkoa wa Songwe, CPA Chausiku Maro ametoa wito kwa watalamu kutoa ushirikiano wa kutosha kwa kutoa maelezo au nyaraka ambazo zinaweza kuzuia kuandika hoja mara wanapokuwa wamefika kufanya ukaguzi.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe, CPA Cecilia Kavishe amesema wamechukua hatua kwa baadhi ya watalamu waliosababisha hati ya mashaka.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe, Mhe. Abrahamu Sambila amesema ataunda timu maalumu kutoka kwa waheshimiwa madiwani na itafundishwa vizuri ili iweze kufuatilia hoja kwa karibu na kuhakikisha Halmashauri haipati hati ya mashaka tena.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.