HATIMA YA MGOGORO WA MPAKA KATI SONGWE NA RUKWA KUJULIKANA KABLA YA SENSA, VIONGOZI KUKUTANA TENA SONGWE
SONGWE: Serikali ya Mkoa wa Rukwa na Songwe zimekubalina kumaliza mgogoro wa mpaka uliodumu kwa takribani miaka 12 kati ya wilaya ya Sumbawanga na Momba kabla ya zoezi la Sensa na makazi kufanyika tarehe 23 Agosti 2022.
Hayo yameibuka kwenye kikao kilichofanyika Julai 18 wilayani Momba baada ya viongozi kutoka sehemu zote mbili kutembelea eneo ambalo lina mgogoro wa mpaka katika kijiji cha Senga wilayani Momba na Ilambo wilayani Sumbawanga.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Joseph J. Mkirikiti amesema baada watalamu kutoka Sumbawanga na Momba kuja kuangalia hali halisi na kupendekeza viongozi wa Mkoa wa Rukwa na Songwe tujionee hali halisi tumekubaliana kabla ya kufika tarehe 23 Agosti mgogoro uwe umetatuliwa.
Akiwa kwenye mkutano wa hadhara, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa amesema mtu pekee mwenye mamlaka ya kugawa mpaka kati ya wilaya na wilaya ni Rais wa Tanzania tu na mpaka unapimwa kwa vipimo tu wala sio hadithi au historia hivyo asitokee mtu yeyote na kujinadi yeye ni bingwa wa mipaka.
Pia, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Joseph J. Mkirikiti amewataka viongozi kuanzia ngazi ya kijiji, kata na Tarafa kutoka wilaya ya Sumbawanga na Momba kuwa mstari wa mbele kulinda na kutunza amani ya maeneo na wasiwe chanzo cha kuanzisha migogoro ambayo haipo kwa wananchi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amesema wananchi wa mikoa yote hawana mgogoro hata kidogo na mpaka wao wanaendelea na kazi zao ila wanachotaka kujua wako sehemu gani ya Mkoa kati ya Songwe au Rukwa ambayo ni hoja ya msingi kwako ukizingatia saizi tunaenda kwenye Sensa ya watu na makazi na miongoni mwa maswali ambayo wataulizwa wanaishi mkoa gani ili Sensa iweze kukamilika.
“Baada ya mto momba kuhama kwenye njia yake kuu changamoto ikawa jinsi ya kutafsiri ya nyaraka za kisheria kati ya Ramani na Tangazo la Serikali la kuanzishwa kwa Mkoa wa Songwe na wilaya ya Momba ipi itumike kutoa uharari wa mpaka” Mhe. Omary Mgumba
Mkuu wa Mkoa amesema pananapokuwa na mgogoro wa kisheria kama huu kuhusu ardhi ni sheria ya ardhi ya vijiji namba 5 na sheria ya ardhi namba 4 ya mwaka 1999 zinaeleza wazi kuwa kwenye mgogoro kama huu kati ya Ramani na Tangazo la serikali kinachotakiwa kufuatwa katika utatuzi wa mgogoro ni Tangazo la Serikali (GN) na sio Ramani.
“Ni kweli mto momba umehama kwenye njia yake kuu na sisi tumejiridhisha pamoja na watalamu lakini wakati wilaya ya Momba inaanzishwa 2012 kupitia Tangazo la Serikali (GN) na Mkoa wa Songwe unaanzishwa 2016 mto momba ulipo sasa ndio ilikuwa ni mpaka kati wilaya ya Momba na wilaya ya Sumbawanga na kati ya Mkoa wa Rukwa na Songwe” Mhe. Omary Mgumba.
Hivyo msingi wa tatizo ili ni wenzetu waliopima vijiji 2007 walifuata ramani 1984 na ya miaka ya nyuma na Serikali ilipoanzisha wilaya ya Momba na Mkoa wa Songwe Ramani hazikuhusishwa kufuata Tangazo la Serikali (GN) ilipotangaza hawakuhuisha Ramani kwa kuzingatie Tangazao la Serikali la kuanzisha wilaya ya Momba na Mkoa wa Songwe kwa kuwa utaratibu Ramani inatakiwa kufuata Tangazao la Serikali amesema Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba.
Mkuu wa MKoa, Mhe. Omary Mgumba ametoa wito kwa wananchi wanaoishi Songwe na Rukwa kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwani mgogoro huu hauna maana yeyote kwao wananchi, hii imewekwa kwa viongozi tu kujua eneo la kiutawala waishie wapi, lakini mwananchi wa kawaida fanya kazi popote na wala haiondoi miliki yako ya mali.
Kwa sasa tumelirudisha kwa watalamu wa ardhi pamoja na wizara ya ardhi waliopima na waliobainisha mipaka ili tarehe 28 Julai 2022 watuambie mpaka utakuwa wapi kwa mujibu wa sheria na badae tutakwenda kuwaambia wananchi ukweli na uhakiki kuwa wapo katika Mkoa wa Rukwa au Songwe kabla ya zoezi la Sensa la watu na makazi.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.