HUDUMA ZA AFYA ZAIMARIKA ZAIDI TUNDUMA.
TUNDUMA: Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluh Hassan imezidi kuboresha huduma za Afya katika Halmashauri ya Mji Tunduma kwa kuongeza zaidi vifaa tiba, watalamu wa Afya pamoja na kuboresha miundombinu ya huduma za Afya.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Fakii Lulandala wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Waziri Kindamba ya ukaguzi wa miradi katika Halmashauri ya Mji Tunduma, Oktoba 7 akiwa katika Hospitali ya Mji wa Tunduma.
Mhe. Fakii Lulandala amesema ujenzi wa vituo vya Afya vya, Chapwa, Chiwezi, Chipaka na Mwaka kati pamoja ujenzi wa hospitali ya Halmashauri ya Mji Tunduma unaonyesha ni jinsi gani Mhe. Samia Suluh Hassan ana nia nzuri ya kuboresha nazingira ya utoaji huduma za afya kwa wananchi wa Tunduma na Wilaya ya Momba.
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji Tunduma, Dkt. Aboubakari Mfaume amesema kitendo cha Serikali ya awamu ya sita kuongeza watumishi wa Afya, kuleta vifaa tiba kama X-ray inasaidie kuimarisha utoaji wa huduma za Afya katika Hospitali ya Tunduma.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Bwn. Philemon Magesa amesema tayari Serikali ya awamu ya sita imeleta fedha milioni 376 za ukamilishaji wa jengo la OPD katika Hospitali hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Waziri Kindamba ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Mji Tunduma kwa kuamua kuanza kutoa huduma katika Hospitali hiyo, kwani hii ndio maana halisi ya Kazi iendelee.
Aidha, Mkuu wa Mkoa amesisitiza watumishi wa Afya watumie lugha nzuri pale wanapotoa huduma kwa wananchi, Mhe. Kindamba amesema eneo la Afya ni eneo ambalo likikosa huduma bora kwa wananchi linaweza kuzalisha kero nyingi kwa wananchi.
Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa, Mhe. Waziri Kindamba amewapongeza viongozi wa Tunduma kwa kufanya kazi kwa kushirikiana katika kuleta maendeleo kwa wananchi na kuwataka waepuka migogoro ambayo inaweza kuwakwamisha.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.