JUHUDI ZAHITAJIKA KUTATUA CHANGAMOTO WANAFUNZI KUHITIMU BILA KUJUA KUSOMA.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Waziri Kindamba amewaagiza wasimamizi wa Elimu kuhakikisha wanatatua changamoto ya wanafunzi kumaliza elimu ya Msingi bila kujua stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu.
Mkuu wa Mkoa alisema Hayo wakati akiongea na wakuu wa Wilaya , wakurugenzi, waratibu elimu Kata pamoja na wadhibiti ubora wa Elimu katika Hafla ya uzinduzi wa Miongozo ya kuboresha elimu Mkoa wa Songwe iliyofanyika Septemba 10.
Alisema miongoni mwa changamoto katika Sekta ya Elimu ni wanafunzi wa darasa la kwanza kuingia darasa la pili bila kumudu stadi za kujua kusoma, kuhesabu na kuandika , Hivyo kusababisha wengine kuhitumu mpaka darasa la Saba bila kujua kusoma.
Mhe. Kindamba amewataka waratibu Elimu Kata kawasimamieni walimu ili wakaongeze nguvu ya kufundisha na kuhakikisha mwanafunzi anayefikia darasa la pili anaweza kumudu stadi tatu za kujua kusoma , kuhesabu na kuandika
"Lengo la Serikali kuanzisha Miongozo ya kuboresha elimu nchini ni kuhakikisha tunatoa wanafunzi Bora ambao wataweza kushindana katika soko la ajira la ndani na nje ya Nchi" alieleza Mkuu wa Mkoa.
Aidha Mkuu wa Mkoa amemwagiza Kamanda wa Polis Mkoa wa Songwe wakishirikiana na wanasheria kuhakikisha wanawakamata na kuwachukulia hatua za kisheria wazazi na walezi wote wanaotelekeza watoto.
"Hii mikoa ya nyanda za juu kusini imekithiri kwa kiasi kikubwa vitendo vya utelekezaji watoto wadogo chini ya miaka mitano na kuwakosesha haki zao za Msingi watoto . Kamanda wa Polis Mkoa hakikisha hili linakomeshwa na wale wote watakao kuwa wanabainika kuchukuliwa hatua Kali za kisheria" alisema Kindamba.
Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Songwe Michael Ligola alisema miongoni mwa sababu zinazopelekea wanafunzi kuhitumu elimu ya Msingi bila kujua kusoma kuwa ni pamoja na uhaba wa walimu madarasa ya awali na darasa la kwanza ambako ndiko kwenye Msingi Mzuri wa kumudu Kkk tatu.
"Mwongozo Unamtaka mwalimu mmoja wa awali aweze kuwafundisha wanafunzi 25, Lakini kwa upande wa Mkoa wetu wa Songwe kutokana na upungufu wa walimu mwalimu mmoja alazimika kufundisha wanafunzi zaidi ya 75 " alieleza Afisa Elimu.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.