Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila amewasili mapema leo asubuhi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe na kupokelewa na watumishi wote.
Mara baada ya mapokezi Kafulila, amepokea taarifa ya makabidhiano ya ofisi kutoka kwa aliyekuwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Herman Tesha katika kikao kifupi cha menejiment ya sekretarieti ya mkoa.
Amesema,“nawashukuru kwa mapokezi mazuri mliyonipa, pili nawapongeza kwa mikakati na mipango mizuri mliyoiweka pamoja na jinsi mlivyokuwa mkichapa kazi”.
Ameongeza kuwa matarajio yake ni kufanya kazi na watendaji na viongozi wote wa mkoa wa Songwe kwa ushirikiano wa pamoja ili kuijenga Songwe kimaendeleo.
Aidha, Kafulila amewashauri wakuu wa sehemu na vitengo wawe wabunifu na wachapakazi ili utumishi wao katika kipindi wakiwa mkoani hapa uwe na matokeo yanayoonekana hasa katika kuinua uchumi na pato la mwananchi.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.