• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
SONGWE REGION
SONGWE REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa MKOA WA SONGWE

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Sehemu
      • Mipango na Uratibu
      • Idara ya Elimu
      • Huduma za Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
  • Wilaya
    • Mbozi DC
    • Songwe DC
    • Momba DC
    • Ileje DC
  • Halmashauri
    • Mbozi
    • Ileje
    • Momba
    • Songwe
    • Tunduma
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Mifugo
    • Madini
    • Kilimo
    • Biashara
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya na Ustawi Wa Jamii
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma ya Mifugo na Uvuvi
    • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
    • Mipango na Takwimu
    • Ujenzi
  • Machapisho
    • Sheria
    • Miongozo
    • Sera
    • Fomu za Maombi
    • Utaratibu
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

KAGUZI ZABAINI ZAIDI YA MADUKA YA DAWA 300 KUKIUKA TARATIBU

Posted on: July 1st, 2021

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kwa Kushirikiana na Mkoa wa Songwe imebaini maduka ya dawa na vifaa tiba 312 ambayo yalikuwa yakiendeshwa kinyume na taratibu na sheria mara baada ya kufanya Kaguzi nne katika kipindi cha Mwezi Septemba 2020 hadi Aprili 2021.

Mfamasia wa Mkoa wa Songwe John Mfutakamba ameyasema hayo jana wakati wa kikao kazi cha  wamiliki na wasimamizi wa Maduka ya Dawa na Vifaa tiba kwa Mkoa wa Songwe ikiwa ni hatua iliyochukuliwa ili kudhibiti uvunjifu wa sheria uliokuwa unajitokeza hapo awali.

Mfutakamba amesema makosa ambayo yamekuwa yakijirudia mara kwa mara ni pamoja na kutozingatia taratibu na sheria za utoaji na uhifadhi dawa na hatua zilizochukuliwa ni baadhi ya maduka kufikishwa mahakamani na kulipa faini ya shilingi milioni sita wa mujibu wa sheria.

Ameongeza kuwa licha ya hatua za kisheria kuchukuliwa Kikao kazi hicho kilicho andaliwa na TMDA kimelenga kuwakumbusha taratibu na sheria wamiliki hao pia Mkoa unapendekeza mafunzo hayo yawe endelevu na yafanyike kwa ushirikiano na Nchi jirani hususani kwa halmashauri zilizoko mpakani.

Kaimu Meneja wa TMDA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Anitha Mshigati amesema lengo la kikao kazi hicho ni kuwakumbusha wamiliki wa dawa na vifaa tiba kanuni za uhifadhi na usambazaji wa dawa kwakuwa wamekuwa wakifanya kaguzi na kuona mapungufu katika maeneo hayo.

Mshigati amesema baadhi ya wamiliki wamekuwa hawana uelewa wa namna ya uhifadhi na utoaji wa dawa na pia katika kutunza kumbukumbu hivyo wameona ni sahihi kuwakumbusha ili wakifanya kaguzi makosa hayo yapungue au kuisha kabisa.

Ameongeza kuwa mara baada ya kikao kazi hicho TMDA itaendelea na kaguzi za mara kwa mara na wanatarajia kukutana na mapungufu kidogo pia dawa na vifaa tiba vilivyopo  Mkoa wa Songwe vitaendelea kupimwa ubora wake kwa kutumia  maabara iliyoko Tunduma pia dawa zinazoingizwa nchini zitapimwa.

Mmiliki wa Duka la Dawa la Suma Israel Mwambene amesema changamoto iliyokuwepo awali ilikuwa ni kukaguliwa bila ya kuwa na elimu ya kutosha ila kupitia mafunzo hayo kuna vitu wamevielewa na hata wakikaguliwa tena watakuwa na uelewa wa kutosha.

Naye Mmiliki wa Duka la Dawa la Daima Israel Mwakilasa amesema kikao hicho kimewawezesha kujua sheria na taratibu ambazo walikuwa hawazifahamu hapo awali.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI January 30, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • RC CHONGOLO AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI WILAYA YA MOMBA KUJADILI HOJA ZA CAG

    June 11, 2025
  • RC CHONGOLO AONGOZA KIKAO CHA KUJADILI HOJA ZILIZO BAINISHWA KATIKA RIPOTI YA CAG HALMASHAURI YA MBOZI

    June 10, 2025
  • RC CHONGOLO APIONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA ILEJE KWA KUPATA HATI SAFI

    June 10, 2025
  • SERIKALI YA SAINI MRADI WA ZAIDI YA BILIONI 119.9 UJENZI WA MRADI WA MAJI TUNDUMA VWAWA

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

ELIMU KWA WATOTO KIPINDI CHA CORONA
Video za Ziada

Kurasa za Karibu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • SALARY SLIP PORTAL
  • AJIRA

Kurasa Mashuhuri

  • IKULU
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE

    Simu: 025 2580305

    Simu ya Kiganjani: 025 2580305

    Barua pepe: ras@songwe.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.