Kikaokazi cha Watendaji na Wataalam wa Afya Mkoani Songwe
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Chiku Gallawa alitoa agizo wakati wa kikaokazi kilichoshirikisha Watendaji na Wataalam wa Afya katika Halmashauri zote Mkoani Songwe kuwa kaya zote zinakuwa na vyoo bora ili kuepusha hatari ya magonjwa ya mlipuko ikiwa ni utekelezaji wa sera ya Afya ya kufikisha asilimia 30 ifikapo mwaka 2020.
Mkuu wa Mkoa alisisitiza kuwa baada ya muda uliotolewa kupita na maagizo hayakufikiwa, Mahakama itahamia katika Vijiji ili kutoa adhabu stahiki kwa watakaokaidi agizo hilo.
Chiku Gallawa alisema usafi wa mazingira unatakiwa ufanyike kila siku katika ngazi ya Kaya na usafi wa utaratibu wa kila Jumamosi ya wiki ya mwisho wa mwezi ni wa kufanya kwenye maeneo korofi kama Madampo, Makaburi, Mifereji na sehemu zingine alisisitiza.
Aidha, Chiku Gallawa akisomewa taarifa ya hali ya Afya ya Mkoa wa Songwe alisema hakuridhishwa na hali ya afya hivyo alimtaka Afisa Afya wa Mkoa George Mgallah kuongeza jitihada kutoa elimu kwa wananchi kabla ya kuanza utekelezaji wa agizo hilo.
Vilevile Mkuu wa Mkoa alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali kuu na Serikali za Mitaa alisema “ Mahali ambapo hakuna ushirikiano kati ya Serikali kuu na Serikali za Mitaa anayeathirika ni mwananchi na tabia hiyo inatokana na ubinafsi wa Watendaji hao na hili tusiliruhusu katika Mkoa wa Songwe” alisema nafasi ya Afisa Tarafa ni Muhimu kwa sababu ana majukumu mawili kwani anatoa taarifa kwa Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri kwa hiyo akitumika vizuri atamsaidia Mkurugenzi kusimamia Kata.
Pamoja na hayo Chiku Gallawa alisema kuwa Mkoa unatafuta vyombo vya usafiri aina ya Pikipiki ili kumfanya Afisa Tarafa kuweza kusimamia kwa urahisi shughuli za Maendeleo katika eneo lake.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.