KILIMO CHA MBOGAMBOGA, MITI YA MATUMDA CHAHIMIZWA SHULENI.
SONGWE: Wajumbe wa Kamati ya lishe Mkoa wa Songwe, wameazimia kila Shule ya msingi na Sekondari kuanza kupanda Bustani za mbogamboga na matunda Ili kuboresha lishe kwa watoto.
Kamati ya Mkoa imetoa wito huo wakati wa kikao cha robo cha lishe cha kupitia utekelezaji wa Afua za lishe kilichofanyika 22 Septemba 2022.
Mjumbe wa Kamati hiyo Charles Chenza amesema kamati iweke azimio la kuitaka kila shule ipande miti ya matunda kama maparachichi, maembe kulingana na hali ya hewa ya shule ni tunda lipi linakubali pamoja na Bustani ya mbogamboga kwa ajili ya lishe kwa wanafunzi.
Naye mwakilishi wa Kamati ya Amani Mch. Rogers Simkonda amesema jamii imekuwa ikipuuza suala la kulima mazao na bustani majumbani mwao na hata kwenye taasisi kama mashule na kuacha maeneo wazi.
"Kwenye taasisi zetu kama mashule hakuna jitihada za kuzalisha chakula kwa ajili ya chakula cha mchana lakini hayo hayafanyiki na hata mazao kama migomba iliyopandwa kwenye maeneo hayo imeanza kuharibika na hakuna ufuatiliaji" amesema Simkonda.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Bi. Happiness Seneda amesema licha ya Mkoa wa Songwe kuwa moja ya mikoa inayozalisha chakula kwa wingi lakini ni miongoni mwa mikoa inayokabiliwa na udumavu unaosababishwa na lishe isiyozingatia ubora.
"Ukosefu wa lishe bora kwa Mtoto ni hatari kwa maisha yake na jamii, hivyo tujitahidi siku 1,000 za mwanzo tuimarishe lishe ikiwemo kuhakikisha mama mjamzito anapata lishe bora na mtoto naye" Bi. Happiness Seneda.
Amesema kuanzia sasa ulimaji wa Bustani na upandaji wa miti ya matunda upewe kipaumbele na kumjengea mtoto tabia ya kulima mbogamboga na matunda tangu akiwa shuleni.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.