KITENGO CHA MANUNUZI CHAKWAMISHA MANUNUZI KWA MIEZI 3 MRADI WASUA SUA, RC MGUMBA ATOA MAELEZO.TUNDUMA:
Manunuzi ya bidhaa mbalimbali za ujenzi wa Kituo cha Afya mwaka kati yamekwama kwa takribani miezi 3 katika kitengo cha manunuzi hali iliyopelekea mradi kwenda kwa kusua sua.Hayo yameibuka tarehe 7 Juni wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba alipofanya ziara ya kukagua mradi wa kituo cha Afya mwaka kati na kukuta moja ya changamoto iliyopelekea mradi kusua sua ni kutokana na mtumishi wa Kitengo cha manunuzi kukaa na madokezo ya manunuzi ya kituo hicho kwa takribani miezi 3 bila kufanya manunuzi.Katibu tawala wilaya ya Momba, Bi. Mary Marcus amesema wasimamizi wa mradi wamefanya malipo ya milioni 16 kununua saruji lakini hadi sasa hawajapata ata mfuko mmoja wa saruji wa kujengea hali iliyopelkea kuuazima saruji ndio ujenzi ukaanza.Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma, Ndg. Josephat Kayombo Amesema mtumishi huyo aliyekaa na madokezo kwa miezi 3 amesimamishwa kazi tayari tangu Aprili 2022 kwa kosa la kuchelewesha ukamilishaji wa miradi baada ya kuona amekuwa kikwazo kwenye miradi mbalimbali ambayo inaendelea kutekelezwa.Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amewataka watalamu wa manunuzi kufahamu sio kila fedha inayokuja lazima wapate, kuna mengine yanafanyika kwa sababu ya mishahara inayolipwa.“Kweli tunakubali kila mbuzi anakula kwa urefu wa kamba yake lakini afisa uyu wa manunuzi kwa kukaa na madokezo miezi 3 yeye ameamua kukata na kamba yake kabisa” Mhe. Omary Mgumba.Mtumishi kama huyu sio wa kumsimamisha kazi tu anapaswa kutumia fedha zake kukamilisha mradi kama ikithibitishwa amefanya ubadhilifu kwenye mradi, amesema Mhe. Omary Mgumba.Mkuu wa Mkoa amesema pamoja na changamoto izo ambazo zimejitokeza swala la kukabidhi mradi wa kituo cha Afya ifikapo Juni 30 uko pale pale watalamu wafanye kazi usiku na mchana.Serikali kuu imeleta fedha milioni 500 fedha za tozo za miamala ujenzi wa kituo cha Afya mwaka kati ambacho kinakwenda kuwaondolea usumbufu wananchi kusafiri umbali wa zaidi KM 8 kufuata huduma.Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa amewataka watumishi kuacha tabia ya kulindana pale wanapoona kuna mwenzao anaaribu kazi kwa maslahi ya Taifa.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.