• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
SONGWE REGION
SONGWE REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa MKOA WA SONGWE

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Sehemu
      • Mipango na Uratibu
      • Idara ya Elimu
      • Huduma za Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
  • Wilaya
    • Mbozi DC
    • Songwe DC
    • Momba DC
    • Ileje DC
  • Halmashauri
    • Mbozi
    • Ileje
    • Momba
    • Songwe
    • Tunduma
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Mifugo
    • Madini
    • Kilimo
    • Biashara
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya na Ustawi Wa Jamii
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma ya Mifugo na Uvuvi
    • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
    • Mipango na Takwimu
    • Ujenzi
  • Machapisho
    • Sheria
    • Miongozo
    • Sera
    • Fomu za Maombi
    • Utaratibu
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

KUTONYONYESHA WATOTO MAZIWA YA MAMA PEKEE KWA MIEZI SITA KUMECHANGIA UDUMAVU

Posted on: August 14th, 2018

   Ongezeko la hali ya udumavu Mkoani Songwe inachagizwa na kuwa ni asilimia 25 pekee ya akina mama wote wanaojifungua ndio huwanyonyesha watoto wao maziwa ya mama pekee kwa muda wa miezi sita.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt. Kheri Kagya ameeleza kuwa udumavu mkoani hapa ni asilimia 37.7 ikiwa na maana kuwa kati ya watu 100, 37 wanatatizo la udumavu kiwango ambacho ni kikubwa licha ya Mkoa Songwe kuwa na Vyakula vya kutosha.

“Moja ya sababu kubwa ya ongezeko la udumavu Mkoani kwetu ni kutokana na akina mama wanaojifungua kutowanyonyesha watoto wao maziwa pekee kwa kipindi cha miezi sita, hali hii huwafanya watoto kukosa virutubisho muhimu katika hatua za awali za ukuaji”, amesema Dkt Kagya.

Ameongeza kuwa maziwa ya mama hujenga afya imara kwa watoto hivyo akina mama wanaojifungua wazingatie ushauri wa wataalamu wa afya wa kunyonyesha watoto maziwa ya mama pekee kwa miezi sita, na kisha kuendelea kunyonyesha na vyakula vingine mbadala mpaka mtoto afikishe umri wa miaka miwili.

Dkt Kagya amesema maziwa yanayopatikana ndani ya saa moja baada ya mama kujifungua yana virutubisho vyote  kwa ajili ya ukuaji wa mtoto hivyo akina mama wazingatie hilo huku akiongeza kuwa ni asilimia 83 ya akina mama wanaojifungua mkoani Songwe huweza kunyonyesha watoto wao ndani ya saa moja.

“Kumekuwa na visingizio kadhaa kwa akina mama kutonyonyesha ndani ya saa moja baada ya kujifungua wengine husema maziwa ya kwanza yenye rangi ya njano kuwa ni machafu, hapana yale maziwa yana virutubisho vingi vya kwa ajili ya afya njema ya mtoto, pia wengine wanasema maziwa pekee hayamtoshi mtoto kwakuwa atasaikia kiu, hilo nalo sio sahihi maziwa ya mama yana kila kitu hata maji pia”, amesisitiza.

Amefafanua kuwa kumekuwa na upotoshaji kuwa mama mwenye Virusi vya Ukimwi akimnyonyesha mtoto atamuambukiza, kitu ambacho sio sahihi.

Mmoja kati ya akina mama anayeishi na Virusi vya Ukimwi Grace Kandonga amesema yeye ana watoto wawili ambapo akijifungua huwa anawanyonyesha maziwa yake pekee kwa miezi sita bila ya kuwapa chakula kingine na wote hawana maambukizi ya VVU.

Bi Kandonga amesema, “huwa nawanyonyesha watoto wangu kwa muda wa miezi sita bila kuchanganya na kitu chochote, baada ya hapo nawapa chakula mbadala kama vile uji na wote wako salama mpaka sasa, kwahiyo nawashauri akina mama wote tuzingatie ushauri wa wataalamu wa afya na watoto wetu watakuwa na afya njema”.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI January 30, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • SERIKALI YA SAINI MRADI WA ZAIDI YA BILIONI 119.9 UJENZI WA MRADI WA MAJI TUNDUMA VWAWA

    March 20, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA ILEJE MHE. FARIDA MGOMI KWA NIABA YA MKUU WA MKOA AFUNGUA HUDUMA YA WIKI YA SHERIA MKOANI SONGWE

    January 25, 2025
  • TASAF MKOA WA SONGWE IMEFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI NA KUJIONEA UTOAJI WA HUDUMA KWA WANUFAIKA WA TASAF MOMBA

    January 03, 2025
  • KIKAO CHA TATHMINI YA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI NA MTOTO MKOANI SONGWE.

    November 07, 2024
  • Angalia zote

Video

ELIMU KWA WATOTO KIPINDI CHA CORONA
Video za Ziada

Kurasa za Karibu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • SALARY SLIP PORTAL
  • AJIRA

Kurasa Mashuhuri

  • IKULU
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE

    Simu: 025 2580305

    Simu ya Kiganjani: 025 2580305

    Barua pepe: ras@songwe.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.