• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
SONGWE REGION
SONGWE REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa MKOA WA SONGWE

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Sehemu
      • Mipango na Uratibu
      • Idara ya Elimu
      • Huduma za Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
  • Wilaya
    • Mbozi DC
    • Songwe DC
    • Momba DC
    • Ileje DC
  • Halmashauri
    • Mbozi
    • Ileje
    • Momba
    • Songwe
    • Tunduma
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Mifugo
    • Madini
    • Kilimo
    • Biashara
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya na Ustawi Wa Jamii
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma ya Mifugo na Uvuvi
    • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
    • Mipango na Takwimu
    • Ujenzi
  • Machapisho
    • Sheria
    • Miongozo
    • Sera
    • Fomu za Maombi
    • Utaratibu
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MADAKTARI BINGWA WABAINI WAGONJWA WA MOYO ZAIDI YA 460 SONGWE

Posted on: April 19th, 2018

  Wagonjwa 467 wenye matatizo ya moyo wamebainishwa na kupatiwa huduma ya ushauri na matibabu kutoka kwa madaktari bingwa waliotoa huduma kwenye kambi maalumu ya siku 4 katika hospitali ya Vwawa-Mbozi Mkoani Songwe.

Timu ya Madaktari Bingwa na wauguzi 5 wameeleza kuwa wagonjwa 18 kati ya hao waliowahudumia wamepewa rufaa ya kufika hospitali za Rufaa kwa ajili ya matibabu Zaidi.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo George Lyego Longopa Kutoka Taasisi ya Magonjwa ya Moyo ya Jakaya Kikwete amesema wameanza matibabu siku ya Jumanne na kila Daktari amekuwa akiona zaidi ya wagonjwa 60 kutokana na hamasa ya wagonjwa waliojitokeza kupata matibabu ya magonjwa ya moyo.

 “Tumeona wagonjwa wengi na tumeamini kuwa Songwe tatizo la Magonjwa ya moyo bado ni kubwa, wagonjwa wengi wamekutwa na matatizo ya shinikizo la damu, moyo kushindwa kufanya kazi vizuri pamoja na matatizo ya mishipa ya damu kuziba”, amesema Dkt Longopa.

Afisa Muuguzi Kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Flora Kasembe ameeleza kuwa mtindo wa maisha ya wananchi wa Songwe unaweza kuwa ni chanzo cha magonjwa ya moyo hasa kutokana na uwepo vyakula vingi lakini wananchi hawali mlo kamili.

Kasembe amefafanua kuwa, “tumekuwa tukitoa elimu ya kuzingatia mlo kamili ili hivi vyakula vingi vilivyopo huku visaidie kuimarisha afya na sio waishie kuuza tu bila wao kutumia, pia wananchi wajenge mazoea ya kufanya mazoezi na endapo watabainika na matatizo na wakaanzishiwa dawa wazitumie kwa usahihi waiache”.

Baadhi ya wagonjwa waliohudhuria kupata matibabu ya moyo wameishukuru serikali kwa kusogeza huduma karibu na utaratibu huo ufanyike mara kwa mara ili wananchi wengi wapate huduma ya madaktari bingwa.

Brigita Haule ambaye amepata matibabu ya moyo ameeleza kunufaika na huduma hiyo kwani hakuwa akifahamu kama ana tatizo la moyo mpaka alipofika katika huduma hiyo.

“Wengi tunajiamini ni wazima kwakuwa hatusikii kuumwa sana ila tunatembea na magonjwa mbalimbali ambayo tunakuja kuyafahamu yakiwa katika hali mbaya, mimi pia sikufahamu kama nina tatizo hivyo nawashauri wote tuwe na utaratibu wa kupima afya zetu”, amefafanua Bi Haule.

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt Kheri Kagya amesema utaratibu wa kuwaalika madaktari bingwa wa moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete uliangaliwa na uongozi wa Mkoa baada ya kubaini kuwa kuna wagonjwa 210 wa moyo.

Dkt Kagya ameongeza kuwa wagonjwa waliojitokeza wamekuwa wengi kuliko matarajio ya awali huku akieleza kuwa hayo ni mafanikio kwakuwa wameweza kuwabaini wagonjwa ambao hawakutambulika hapo awali.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI DATA CLEARK, CLINICIAN NA NURSE October 01, 2021
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • WANAWAKE WAGUSA MAISHA YA WATU WENYE WAHITAJI

    March 08, 2023
  • WITO WATOLEWA WANAWAKE KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI ZILIZOPO.

    March 06, 2023
  • NIMEKUJA KUBORESHA MAZURI YOTE, RC MICHAEL.

    March 03, 2023
  • TUTAFANYA KAZI NA WADAU WOTE KUTIMIZA LENGO LA SERIKALI: RC MICHAEL.

    March 02, 2023
  • Angalia zote

Video

ELIMU KWA WATOTO KIPINDI CHA CORONA
Video za Ziada

Kurasa za Karibu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • SALARY SLIP PORTAL
  • AJIRA

Kurasa Mashuhuri

  • IKULU
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE

    Simu: 025 2580305

    Simu ya Kiganjani: 025 2580305

    Barua pepe: ras.songwe@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.