• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
SONGWE REGION
SONGWE REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa MKOA WA SONGWE

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Sehemu
      • Mipango na Uratibu
      • Idara ya Elimu
      • Huduma za Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
  • Wilaya
    • Mbozi DC
    • Songwe DC
    • Momba DC
    • Ileje DC
  • Halmashauri
    • Mbozi
    • Ileje
    • Momba
    • Songwe
    • Tunduma
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Mifugo
    • Madini
    • Kilimo
    • Biashara
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya na Ustawi Wa Jamii
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma ya Mifugo na Uvuvi
    • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
    • Mipango na Takwimu
    • Ujenzi
  • Machapisho
    • Sheria
    • Miongozo
    • Sera
    • Fomu za Maombi
    • Utaratibu
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MAKAMU WA RAIS AZINDUA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2019 MKOANI SONGWE

Posted on: April 3rd, 2019

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa rai kwa Wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutumia mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2019 kumkumbuka Baba wa Taifa kwa kupinga vitendo vya dhulma, ufisadi, rushwa, maradhi, chuki, dharau na kuwataka kuenzi umoja na mshikamano wetu kuchapakazi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo kwenye sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge Kitaifa zilizofanyika kwenye uwanja wa Kimondo uliopo Mlowo mkoani Songwe na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali akiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

Kaulimbiu ya mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019 ni “Maji ni haki ya kila mtu, tutunze vyanzo vyake na tukumbuke kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa”

“Nimependezwa na kaulimbiu hii ambayo ina uwiano wa moja kwa moja na jukumu langu la kila siku la kusimamia na kutunza mazingira ya nchini, Sote tunafahamu kuwa bila utunzaji thabiti wa mazingira basi vyanzo vya maji hupotea” alisema Makamu wa Rais

Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama nchini inaendelea kuimarika ambapo huduma ya maji vijijini  imeongezeka kutoka wastani  wa asilimia 58.7 kwa mwaka 2018 hadi kufikia asilimia 64.8 mwezi februari 2019 na miji mikuu ya mikoa kutoka asilimia 78 mwezi machi 2018 mpaka asilimia februari 2019.

“Niwahakikishie wananchi tutatekeleza kwa vitendo ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi inayo tutaka kuboresha huduma ya maji vijijini kufikia asilimia 85 na mijini kwa asilimia 95 ifikapo 2020” alisisitiza Makamu wa Rais

Aidha, Makamu wa Rais kupitia hadhara ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019 ametoa wito kwa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuacha kufanya shughuli za kibinadamu kama vile kilimo, ufugaji, ujenzi, ukataji na uchomaji miti kwenye vyanzo vya maji.

Makamu wa Rais pia amewakumbusha wananchi juu ya uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika mwezi oktoba 2019 kuhakikisha wanachagua Viongozi wachapakazi na wenye dhamira ya maendeleo kwa jamii.

Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019 zitaongozwa na Ndugu Mzee Mkongea Ali kutoka Mjini Magharibi.



(Picha/Habari-Ofisi ya Makamu wa Rais)

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI January 30, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • SERIKALI YA SAINI MRADI WA ZAIDI YA BILIONI 119.9 UJENZI WA MRADI WA MAJI TUNDUMA VWAWA

    March 20, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA ILEJE MHE. FARIDA MGOMI KWA NIABA YA MKUU WA MKOA AFUNGUA HUDUMA YA WIKI YA SHERIA MKOANI SONGWE

    January 25, 2025
  • TASAF MKOA WA SONGWE IMEFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI NA KUJIONEA UTOAJI WA HUDUMA KWA WANUFAIKA WA TASAF MOMBA

    January 03, 2025
  • KIKAO CHA TATHMINI YA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI NA MTOTO MKOANI SONGWE.

    November 07, 2024
  • Angalia zote

Video

ELIMU KWA WATOTO KIPINDI CHA CORONA
Video za Ziada

Kurasa za Karibu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • SALARY SLIP PORTAL
  • AJIRA

Kurasa Mashuhuri

  • IKULU
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE

    Simu: 025 2580305

    Simu ya Kiganjani: 025 2580305

    Barua pepe: ras@songwe.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.