MALIPO YA MILIONI 511 BILA RISITI ZA EFD ZAWAWEKA PABAYA WATUMISHI.MBOZI
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mbozi kumpatia maelezo ndani siku 2 kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi na Uhasibu kwa nini walifanya malipo ya zaidi milioni 511 kwa watoa huduma bila uwepo wa risiti za kielotriniki za (EFD) kwa mwaka wa fedha 2020/2021.
Mkuu wa Mkoa ametoa maagizo hayo wakati wa Baraza la kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kilichofanyika 18 Juni 2022.Mkuu wa Mkoa amesema manunuzi na malipo kwa watoa huduma ambao hawana risiti za kielotriniki (EFD) zaidi ya thamani ya Milioni 860 na baada ya kuwasilisha risiti zimebaki Milioni 511 ambazo risiti zake hazijawasilishwa.
"Kwenye hili mumeonyesha dharua kubwa kwa Serikali na viongozi kwa sababu maelekezo yaliishatolewa, kama mtu hana EFD risiti malipo yasifanyike lakini bado nyie mumelipa" Mhe. Omary Mgumba.
Pamoja na kutoa maelekezo ndani ya siku 2, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba ameagiza hatua za kinidhamu zichukuliwe kwa watu wa fedha na manunuzi pamoja na watumishi wote waliohusika kuruhusu malipo ya zaidi Milioni 511 bila uwepo wa risiti za kielotriniki
Mkuu wa Mkoa amesema jambo hili lina upotevu wa fedha za Serikali na viashiria vya malipo hewa ya Serikali ndio maana kuna ukosefu wa risiti za kielotriniki za EFD.
Wakati huo huo amepiga marufuku Serikali kufanya kazi na Kampuni au mfanyabiashara ambaye hajasajiliwa na GPSAMWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.