Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Songwe zilianza Aprili 11, 2017 katika Wilaya ya Momba ambapo miradi 18 iliwekwa Mawe ya Msingi na kuzinduiliwa kati ya miradi hiyo 7 ilikuwa katika Halmashauri ya Momba na 11 katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma.
Miradi iligharimu Jumla ya Shilingi 3,973,000,000.00 kutoka Serikalini na Shilingi 11,272,400.00 mchango wa Wananchi.
Aidha hali ya upimaji wa VVU/UKUMWI kwa hiari wakati wa mkesha wa Mwenge ilionesha kuwa watu wazima 27 kati ya hao kiume 9 na Wanawake 18 walipata maambukizi kati ya watu 567 waliopimwa. Kati ya hao watu wazima walikuwa 496 ambapo 269 walikuwa Wanaume na 287 Wanawake sawa na maambukizi kwa 5%. Watoto 71 walipima, kati ya hao Wavulana walikuwa 35 na Wasichana 36 na hakuna mtoto aliyeonesha kuwa na maambukizi.
Ili kupunguza maambukizi mapya watu 798 walipata ushauri na kugawiwa Kondomu kati ya hao wanaume walikuwa 619 na Wanawake 197. Jumla ya Kondomu 7,182 zilisambazwa.
Mwenge ulikabidhiwa katika Halmashauri ya Ileje Aprili 13, 2017. Jumla ya miradi 5 ilizinduliwa, kufunguliwa na kukaguliwa ikiwa na thamani ya Shilingi 395,299,000.00
Wakati wa mkesha wa Mwenge watu 446 walipima VVU/UKIMWI kati ya hao wanaume 360 na Wanawak 106. Maambukizi yalikuwa wanaume 4 na Wanawake 2 jumla 6 ambapo ni sawa na asilimia 1.5 ya maambukizi.
Mwenge ulikabidhiwa katika Wilaya ya Mbozi ambapo miradi 6 ilikaguliwa, zinduliwa na kuwekwa mawe ya msingi yenye jumla ya Shilingi 3,016,656,250 kwa mchanganuo wa Shilingi 8,877,000 kutoka Serikali kuu, 1,775,400 kutoka Halmashauri ya Wilaya, 686,003,850 mchango wa Jamii na 2,320,000,000 kutoka kwa Wafadhili.
Mwsho Mwenge ulikimbizwa katika Wilaya ya Songwe ambapo miradi 5 ilipitiwa yenye thamani ya Shilingi 564,389,160. fedha hizo zilitokana na michango kutoka Serikali kuu Shilingi 179,255,000, Halmashauri ya Wilaya 42,000,000, Jamii 70,515,160 na Wafadhili 272,619,000
Aidha, zoezi la upimaji VVU/UKIMWI lilifanyika katika eneo la mkesha ambapo watu 430 walipima damu kati ya hao Wanaume walikuwa 220 na Wanawake 210. Hali ya maambukizi ilikuwa wanaume 11 na wanawake 4 jumla watu 15 sawa na asilimia 3.
Ili kupunguza maambukizi mapya ya VVU/UKIMWI elimu juu ya matumizi ya kondomu ilitolewa ambapo mipira ya kiume (Kondomu) 12,960 zilitolewa kwa wanaume na 150 kwa wanawake.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.