MBOZI YAFUNGA MWAKA KWA MIKOPO YA MILIONI 740.
MBOZI: Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi katika mwaka wa fedha 2021/2022 imefanikiwa kutoka mikopo ya milioni 740,750,000 kwa vikundi 94 vya wanawake, vijana na walemavu.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mbozi, Bi. Melania Kwai amesema hayo Julai 29, katika hafla ya kukabidhi mikopo ya thamani ya milioni 242,400,00 kwa robo ya nne (4) ya mwaka wa 2021/222, hafla ambayo imepambwa na Baraza la Madiwani la Mbozi.
Mlemavu moja, Bwn. Samwel Sampamba amejipatia mkopo wa thamani ya milioni 8,300,000 ambayo amenunua bajaji moja na hii ni baada ya Serikali kurekebisha sheria kuruhusu mlemavu ata akiwa moja aweze kupata mkopo kutokana na ugumu uliopo kupata kikundi cha watu wenye ulemavu ambao wako sehemu moja na wanafanya kazi za aina moja, amesema Afisa Maendeleo ya Jamii, Bi. Melania Kwai.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Mhe. George Musyani amesema mikopo inayotolewa sio ya bure, sio sadaka au hisani ila inapaswa kurejeshwa ila watu wengine waweze kukopeshwa na Halmashauri yao ya Mbozi.
Mhe. George Musyani amesema kiu ya Halmashauri ni kuona wote waliopata mikopo watakwenda kuinua maisha yao kiuchumi
Mwaka 2021/2022 Halmashauri ilitakiwa tutoe Milioni 270 kutokana na Bajeti yetu lakini tumetoa mkopo zaidi ya milioni 740 kwa sababu tulipata marejesho ya mikopo ya zaidi milioni 400 ambazo tumeamua kuzikopesha tena kwa vikundi na kufikisha milioni 740,750,000 amesema Mwenyekiti wa Halmashauri, Mhe. George Musyani.
Katibu Tawala Wilaya ya Mbozi, Bi. Tusubilege Benjamin amesema Serikali haitegemei kabisa kuona vyombo vya moto vilivyokabidhiwa vikutwe kwenye matukio ya uharifu, kwani kikikamatwa ata chombo kimoja kwenye vitendo vya uharifu basi kikundi kizima kitawajibika na uharifu huo pamoja na ayetumia chombo hicho.
"Serikali inawataka vijana wavitumie kwenye malengo yaliyokusudiwa na sio vitendo vya uharifu" Tusubilege Benjamin.
Mwenyekiti wa kikundi cha Hapa Kazi tu, Said Lwenje ambaye kikundi chao kimepata milioni 12,500,000 ambazo wamenunua pikipiki 5 amesema watajitahidi kufanya marejesho kwa wakati kabla ata ya mwaka kwa kuwa kazi zipo kila siku na Serikali imewapatia vitendea kazi.
Lwenje amesema kila siku watakuwa wanazikagua pikipiki kabla ya kuanza kazi na mwisho wa kufanya kazi kwa kikundi chao ni saa 2 usiku na pikipiki za kikundi hakuna kubeba magendo au bidhaa ambazo Serikali imepiga marufuku.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Mhe. George Musyani amesema lengo la Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ni kutoa mikopo yenye thamani ya Bilioni 1 kama marejesho yatafanyika vizuri na ukusanyaji wa mapato ukifanyika vizuri pasipo kuruhusu mapato Kuchepushwa.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.