Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Ndg.John Mwaijulu, amefungua mafunzo rasmi Tarehe 21 Agosti 2023 ya mfumo mpya wa Ununuzi wa umma kwa njia ya mtandao (National e-Procurement System of Tanzania-NeST).
Mafunzo hayo yataendelea hadi 25 Agosti 2023. Wakuu wa idara,Vitengo na Utumishi kutoka katika Halmashauri zote tano(5) za Mkoa wa Songwe wameshiriki katika mafunzo hayo. Mafunzo hayo yanatolewa na wataalamu Kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa ,na baadhi ya taasisi zimeshaanza kutumia mfumo wa NeST tangu tarehe 1 Julai 2023. Mpango ni kuhakikisha ifikapo tarehe 1 Oktoba 2023, Ununuzi wote wa umma Unafanyika kupitia mfumo wa NeST na si vinginevyo.
Mfumo huu mpya utahitaji wazabuni pamoja na wanunuzi kujisajili katika mfumo wa Ununuzi na kufanya shughuli zote za Ununuzi Wa umma kupitia Mfumo wa NeST.Lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo wakuu wa idara,vitengo na Utumishi ili waweze kufanya Ununuzi Wa umma kwa njia ya mtandao kupitia NeST. Hatua hii inalenga kuboresha uwazi, ufanisi, na uwajibikaji katika mchakato wa Ununuzi Wa serikali katika mkoa wa Songwe.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.