Mkuu wa mkoa wa Songwe Mhe. Dkt Francis Michael amewakilishwa na Mkuu wa wilaya Ya Mbozi Mhe.Esther Mahawe katika kuu kabithi Mwenge wa Uhuru kwa mkoa wa Mbeya ambapo mkuu wa mkoa wa Mbeya amewakilishwa na mkuu wa wilaya ya Mbeya Mhe. Beno Malisa
Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mhe. Esther Mahawe, amewapongeza wakimbiza Mwenge Wa Uhuru kitaifa kwa niaba ya Dkt. Michael na kutoa ahadi kama Mkoa kumalizia marekebisho yaliyotolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa, Ndg. Abdalla Shaib Kaim katika halmashauri zote tano za mkoa wa Songwe.
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Bi Happiness Seneda (wa pili kushoto) ameshiriki makabidhiano ya Mwenge wa uhuru kitaifa kutoka Mkoa wa Songwe Kwenda MKoa wa Mbeya wakiagwa na Moja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Bi Atupokile Elia Mhalila.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.