MKOA WA SONGWE WATAKIWA KUWEKEZA KATIKA MATUMIZI YA NISHATI SAFI.
Posted on: September 19th, 2024
Naibu Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Bi. Christina Solomon Mndeme amewataka Viongozi wa Mkoa wa Songwe kusisitiza wananchi na taasisi kutumia nishati safi ili kupunguza uharibulifu wa mazingira.
Bi. Mndeme ametoa agizo hilo leo Alhamisi Septemba 19, 2024 wakati wa Mkutano Nishati Safi na Uhifadhi wa Mazingira kwa Mkoa wa Songwe.
Mkutano Huo ambao umehudhuriwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Bi. Happiness Seneda umewahusisha viongozi mbalimbali wa ngazi ya mkoa, wilaya za mkoa wa Songwe, kata na wadau mbalimbali ndani ya Mkoa huu.