Mkuu wa mkoa wa Songwe Chiku Galawa amezindua rasmi zoezi la uandikishaji watu na makazi katika mfumo wa kielektroniki (ePRS) mkoani Songwe.
Mkuu wa mkoa huyo amesema kuwa, katika zoezi hilo jumla ya watu laki 998,000 wanataraji kuandikishwa, mfumo ambao umenza kwa wakazi laki 414,000 katika kaya 117,000 katika wilaya ya Mbozi.
Amezitaja faida za zoezi hilo kuwa ni pamoja na kusogeza huduma kwa jamii kulingana na idadi yao, na pia itasaidia kuwa na kumbukumbu sahihi kuanzia ngazi ya kitongoji hadi taifa kwa ujumla.
Mpango huo wa uandikishaji ambao ulianzia majaribio wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani unatarajia kufanyika wilaya zote za mkoa wetu wa Songwe ambapo utafanyika ndani ya siku 29.
Alisema kuwa uandikishaji kidigitali Mkoani Humo umeanza katika Kata 8 kati ya 29 za Wilayani Mbozi ambapo unatarajia kufanyika katika mkoa mzima wa Songwe ili kupata takwimu sahihi za wakazi wa mkoa huo.
Hata hivyo, aliongeza kuwa baada ya kuanza zoezi la Uandikishaji, mambo mengi yamebainika ikiwemo watoto wadogo chini ya miaka 18 kuwa wakuu wa kaya, licha ya zoezi hilo kuwa na mwitikio ni mkubwa.
Mpango huo wa uandikishaji unafadhiliwa na Shirika la kuhudumia watoto Duniani UNICEF kupitia chuo cha Takwimu cha Afrika Mashariki, kilichopo jijini Dar es salaamu, kazi ambayo inaratibiwa na Ofisi ya Takwimu ya Taifa.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.