Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dkt Francis Michael, amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Frida Mgomi kuhakikisha anamrejeaha shuleni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya wasichana (Ileje Girls) anayedaiwa kukatisha masomo na kwenda kufanya kazi za ndani ili aendelee na masomo.
Pamoja na hilo, Dkt. Michael
pia ameagiza
Kurejeshwa shuleni hapo kwa wanafunzi wengine watatu ambao wazazi wao
waliwahamisha na kuwapeleka katika shule za kutwa kwa kisingizio cha wazazi kukosa michango ya chakula.
Mkuu wa mkoa Dkt. Michael, Ametoa maagizo hayo November 14, 2023, wakati akitimiza ahadi yake ya kuwapatia kila mwanafunzi daftari tano (Counter book) wanafunzi wote wa shule hiyo.
Awali akitoa taarifa ya shule, Kaimu Mkuu wa shule hiyo, Sharon Kadinde, alisema shule hiyo ya wasichana iliyoanzishwa mwaka huu ilipangiwa wanafunzi 75 , lakini walioripoti shuleni hapo ni 71 tuu.
Aliongeza kuwa mwanafunzi mmoja alikatiza masomo kwa shinikizo la wazazi wake, huku wanafunzi wengine watatu akidai kuwa, licha ya kuripoti shuleni hapo wazazi wao waliwahamisha na kuwapeleka katika shule za kutwa kwa madai ya kutokuwa na uwezo wa kuchangia chakula.
" Baada ya wazazi wake kumshinikiza aacha shule, tulifuatilia na kubaini kuwa mwanafunzi huyo kwa sasa anafanya kazi ndani katika mji wa Tunduma . Alieleza Kaimu Mkuu wa shule hiyo.
Kufuatia taarifa hiyo, Mkuu wa Mkoa alimtaka mkuu wa wilaya hiyo, kuwafuatilia wazazi wa mwanafunzi huyo ili wamrudishe mwanafunzi huyo aendelee na masomo.
" Mwanafunzi huyu atakapo rudi shule Mkurugenzi hakikisha unampatia mchango huo wa chakula ili aweze kutimiza ndoto zake za kupata elimu.. tena nimeambiwa mwanafunzi huyo ana uwezo mkubwa darasani" alisisitiza Mkuu wa Mkoa.
Katika hatua nyingine, Dkt. Michael imewaonya wazazi wenye tabia za kuwakatisha masomo Wanafunzi amewataka kuacha mara moja kwa sababu watakaobainika watakamatwa na kuchukuliwa Hatua kali za kisheria.
Baadaya ya maelekezo hayo, Mkuu wa Mkoa alikagua Maendeleo ya Ujenzi wa majengo mawili ambayo ni nyumba moja ya Mwalimu itakayotumiwa na familia mbili, inayogharimu kiasi cha sh. Milioni 100 ambazo ni fedha kutoka serikali Kuu.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.