Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mheshimiwa Dkt. Francis Michael ameongoza kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Songwe kilicho husisha Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na wakala wa barabara Vijijini na Mjini(TARURA).
Kikao hicho kimefanyika leo Jumanne Machi 05, 2024 katika ofisi za Mkoa za Mkuu wa Mkoa huyo zilizopo Nselewa, Mbozi.
Kikao hicho ambacho pia kimehudhuriwa na Katibu Tawala wa Mkoaa huo, Bi. Happiness Seneda,Wakuu wa Wilaya, Wenyeviti wa halmashauri, Wabunge na Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Suleman Bishanga, kimewahusisha wakuu wa Taasisi za Serikali za Mkoa kamati ya Usalama ya mkoa na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Mkoa wa Songwe.
Kikao hicho kimejadili jitiha na mbinu mbalimbali katika kuboresha miundombinu ya barabara katika mkoa wa Songwe.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.