Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela ametoa siku saba kwa Mtendaji wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mlowo kuhakikisha mji huo unakuwa safi.
Brig. Jen. (Mst) Mwangela ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wananchi wa Mlowo na kupokea kero, maoni na malalamiko yao ambapo kero kubwa ya wananchi ilikuwa ni uchafu kutokana na magari ya kukusanya taka kutokusanya taka kwa wakati.
“Mlowo ni mji wa Kibiashara unatakiwa utunzwe vizuri, uwe msafi na upangike, natoa wiki moja Mtendaji wa Mji wa Mlowo hakikisha mji unakuwa msafi nami nitapita kukagua mwenyewe”, ameelekeza Brig. Jen. (Mst) Mwangela
Katika Mkutano huo Brig. Jen. (Mst) Mwangela amewapongeza wananchi wa Mlowo kwa kujitokeza kwa wingi katika Uzinduzi wa Kitaifa wa Mbio za Mwenge wa Uhuru uliofanyika kitaifa Mkoani hapa katika uwanja wa Kimondo uliopo Forest Mlowo Aprili 2, 2019.
Amesema hamasa walio ionyesha katika tukio hilo la kitaifa imeupa hadhi na heshima mkoa wa Songwe na hivyo kuahidi kuwa endapo yatatokea matukio mengine ya kitaifa yatakayofanyika Mkoani Songwe, Mlowo itapewa kipaumbele.
Brig. Jen. (Mst) Mwangela aliongeza kwa kuwataka wajasiriamali wadogo wa Mlowo kuchukua vitambulisho ili watambulike na serikali pia akawasihi wananchi kuwapa kipaumbele wajasiriamali wadogo wenye vitambulisho kwa kununua bidhaa na kutumia huduma zao.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.