Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Daniel Chongolo, amefanya Ziara katika Wilaya ya Mbozi Tarehe 04 Novemba 2024, kwa ajili ya kukagua maendeleo ya miradi ya maji. Ziara hii imelenga kuhakikisha miradi inayotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira ya Vwawa-Mlowo inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa katika wilaya ya Mbozi, Mkoani Songwe.
|
Moja ya mradi Uliokaguliwa ni mradi wa ukarabati wa vyanzo vya maji vya Mwansyana unaotekelezwa na kampuni ya HAMWA Construction Co. Ltd. Mradi huu wenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.776.
Mpaka sasa, mradi huo umekamilika kwa asilimia 88, huku asilimia 80 ya malipo yakiwa yameshatolewa. Kazi zilizotekelezwa ni pamoja na ununuzi wa mabomba yenye urefu wa mita 17,400, na kazi zilizo pangwa kufanyika ni ufungaji wa washouts na air valves, na ununuzi wa vifaa kama pikipiki na kompyuta. Mradi huu unatarajiwa kunufaisha wananchi wapatao 13,107 katika Wilaya ya Mbozi. ambapo kwa sasa Mradi unazalisha lita laki nne hadi laki sita za maji kwa siku. Kukamilika kwa mradi huu kutapelekea uwezo wa kuzalisha lita milioni 1.4 kwa siku.
Mhe. Chongolo amemsisitiza mkandarasi kumalizia kazi zilizosalia kwa haraka ili wananchi waweze kupata huduma za maji safi na salama kwa wakati. Pia, ametoa wito kwa mamlaka husika kuhakikisha miradi yote ya maendeleo inasimamiwa kwa ukaribu ili kufikia malengo ya serikali ya kuwahudumia wananchi na Kumtua Mama Ndoo Kichwani.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.