MSITEGEMEE TOFALI KWENYE KIWANDA CHENU TU TAFUTENI KWINGINE, RC MGUMBATUNDUMA:
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba ameitaka Halmashauri ya Mji wa Tunduma kutokutegemea tofali kwenye kiwanda chao tu badala yake watafute tofali sehemu nyingine yeyote ili miradi ya ujenzi ikamilike haraka kabala ya kufika 30 Juni 2022.Mkuu wa Mkoa ametoa agizo ilo leo Juni 7 wakati wa ziara ya ukaguzi wa mradi wa madarasa kumi (10) ya gorofa katika shule ya msingi Haisoja na kukuta mradi umekwama kwa madai ya kusubiria tofali kutoka kwenye kiwanda cha Tunduma.“Kama kiwanda cha Tunduma kimeishiwa tofali katafuteni sehemu nyingine kwani kiwanda cha Tunduma nacho kinafanya biashara kama wafanyabiashara wengine ni marufuku kusubiria tofali wakati mradi umekwama wakati tofali sehemu nyingine zipo” Mhe. Omary Mgumba.Wafanyabiashra wote ni wa Serikali ndio maana Mhe. Samia Suluh Hassan amefungua uchumi wa nchi kila mtu mwenye vigezo anaweza kufanya kazi na Serikali, hivyo awe mtu binafsi au Serikali kama ana vigezo lazima afanye kazi na Serikali amesema Mhe. Omary Mgumba.Aidha, Mkuu wa Mkoa amesema tofali inaponunuliwa sehemu yeyote ile lazima ipimwe kabla ya kutumia kama ina ubora hii haijarishi unachukua tofali kwenye kiwanda cha Serikali au cha binfasi lazima zipimwe kwa kuzingatia ubora wake.Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa amekataa mkataba mpya aliongozewa mkandarasi na Halmashauri wa miezi mitatu (3) ambao ulimtaka akamilishe ujenzi Septemba 2022 badala yake Mkuu wa Mkoa amemtaka mkandarasi akamilishe ujenzi ifikapo Juni 30 kama ilivyo maelezo ya Serikali na kumtaka mkandarasi afanye kazi usiku na mchana kwa kufunga taa eneo la mradi.Halmashauri ya Mji wa Tunduma imejenga madarasa kumi (10) ya gorofa katika Shule ya msingi Haisoja kwa thamani ya shilini Milioni 450 madarsa ambayo yanakwenda kutatua changamoto ya msongamano wa wanafunzi madarasni kwa shule za mji wa Tunduma.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.