ILEJE: Kutokana na kuongezeka kwa matukio ya watendaji wa vijiji na Kata kula fedha mbichi kwenye Halmashauri na baadhi ya maeneo inaonekana kuwa ni mtandao.Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omary Mgumba amewataka watendaji wote ambao wanakusanya fedha za Halmashauri kupitia POS kufuata utaratibu wa kuweka fedha Benki mara anapokusanya na ikitokea kuna kiongozi wake anahitaji fedha ahakikishe anayempatia fedha unamsainisha.Mkuu wa Mkoa amesisitiza kuwa awe Mkurugenzi au Mkuu wa Idara anakwambia niletee fedha akikisha unamsainisha na kama ujafanya hivyo tukikukamata usituambie fedha alichukua flani wakati utaratibu wa fedha unaujua ukikusanya weka Benki."Wakati flani unaona Mtendaji wa Kijiji unaambiwa anadaiwa Milioni 10 au 20 lakini ukimwangalia unaona maisha yake hayalingani na izo fedha" Omary Mgumba.Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa watendaji kuendelea kufuata taratibu za fedha wakikusanya na wapeleke Benki ili anayehitaji aende kuchukua Benki na sio mkononi mwa Mtendaji
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.