MWANAFUNZI APATA TZS 103,000 KISHUJAA ALIPOJITOKEZA KWA MGENI RASMI.SONGWE:
Mwanafunzi wa darasa la tatu Shule ya Msingi Lulu, Nikodem Ndimbwa amepata fedha kiasi cha 103,000 baada ya kujitokeza kwa mgeni rasmi apate zawadi ya vifaa vya shule wakati sio miongoni mwa wanafunzi ambao walikuwa kwenye orodha ya kupata zawadi.
Mwanafunzi huyo aliibuka kwa mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika ambayo kwa ngazi ya Mkoa yamefanyika viwanja wa CCM-Mbozi, 16 Juni 2022.Ameibukia kwa mgeni rasmi akiwa hana sare za Shule uku akionekana ni mtu mwenye uhitaji wa vifaa vya Shule ambavyo aliona wenzake wakipata kutoka kwa muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Songwe, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Faki Lulandala.
Mwenyekiti wa Halmahera ya Wilaya ya Ileje, Mhe. Ubatizo Songa alivyomuona mwanafunzi uyo alilazimika kumuomba mgeni rasmi kufanya jambo juu ya mtoto huyo.
"Mhe. Mgeni rasmi nimeguswa na mtoto huyu tunaomba tufanye jambo na mimi naanza na shilingi 10,000 ameonekana ni mwenye mahitaji" Mhe. Ubatizo Songa.
Mgeni rasmi wa maadhimisho ya siku ya Mtoto Afrika, Mhe. Faki Lulandala akaruhusu jambo ilo lifanyike kwa wageni waliohudhuria na likiratibiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje aliyeleta hoja.
Kisha, Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Faki Lulandala akamkabidhi Mwalimu anakosoma mwanafunzi huyu kiasi cha fedha shilingi 103,000 na kumuagiza ahakikishe mtoto anapata mahitaji muhimu ya shuleni kwanza.
Pia, Mhe. Lulandala amemuagiza Mwalimu huyo kufika hadi Nyumbani kwa mwanafunzi kuangalia mazingira ya Nyumbani kwao na kama kuna mahaitaji mengine zaidi basi ayawasilishe Serikalini kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mbozi kwa ajili ya hatua zaidi ya kumsaidia mwanafunzi huyo.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.