Wavuvi na wachimba madini wadogowadogo wamepewa muda wa siku nane kuchukua vitambulisho vitakavyo wawezesha kutambulika rasmi kama wajasiriamali wadogo wadogo ili waweze kufanya shughuli halali za uzalishaji mali bila kusumbuliwa.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela ametoa maelekezo hayo mapema wiki hii akiwa ziarani Wilayani Songwe ambapo ametembelea kambi ya wachimbaji wadogo wa madini katika Kijiji cha Saza na wajasiriamali wa uvuvi katika kambi ya sabasaba pembezoni mwa mto Rukwa.
Brig. Jen. (Mst) Mwangela amesema, “mjasiriamali mdogomdogo unayefanya shughuli yeyote halali inayokuingizia kipato na hulipi kodi TRA serikali inataka kukutambua hivyo basi unatakiwa kuchukua kitambulisho ili usisumbuliwe”.
Aidha amezitaka halmashauri za Mkoa wa Songwe kuhakikisha zinasimamia vizuri ugawaji wa vitambulisho vya wajasiriamali wadogo ili kuepuka udanganyifu na kuhakikisha kila mjasirimali anatambulika kwa kupata kitamblisho hicho.
Naye Afisa Kodi Kutoka Mamlaka ya Mapato nchini TRA Omary Iddi amesema wajasiriamali wadogowadogo ambao kipato chao kwa siku wanapata chini ya shilingi milioni nne kwa mwaka wanapaswa kuchukua kiambulisho cha Ujasiriamali ili nao waweze kuchang pato la taifa.
Wajasiriamali wadogo wanaoishi kwenye kambi ya uvuvi ya Sabasaba, Wachimbaji wadogo wa madini wa Saza na wajasiriamali wegine Wilayani Songwe wamezipongeza juhudi za serikali za kuweka mazingira mazuri ya ulipaji kodi kwa manufaa ya maendeleo ya Taifa.
Simkonda Maiko amesema anaipongeza serikali kwa kuwatambua wajasiriamali wadogo wadogo na hivyo kuwawekea utaratibu mzuri wa kuchangia mapato pia itawasaidia kutosumbuliwa.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.