NGUVU IMEONGEZWA KWA WAHAMIAJI HARAMU DHIDI YA TISHIO LA EBOLA, RC KINDAMBA.
TUNDUMA: Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Waziri Kindamba amesema vyombo vya ulinzi vimejipanga kuhakikisha mipaka ya Nchi inakuwa imara na salama na wanadhibiti wahamiaji haramu wanao tumia njia zisizo halali kuvuka katika mipaka yote wa Tunduma kwa Nchi ya Zambia na Isongole kwa Nchi ya Malawi.
Mhe. Kindamba amesema hayo, Oktoba 7 akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wakati wa ukaguzi eneo linalotumika kwa wasafiri wanaoingia na kutoka Nchini katika mpaka wa Tunduma alipofika kuona jinsi mipango ya Serikali inavyotekelzwa kuhakikisha Kila mgeni anapimwa dhidi ya tishio la ugonjwa wa Ebola ambao umeripotiwa nchini Uganda.
Nami nimejiridhisha jinsi watalamu wa Afya wa Songwe walivyojiandaa katika kupambana na tishio la Ebola kuhakikisha Kila msafiri anachunguzwa na kama kwa bahati mbaya akipatikana wamejipanga vizuri kuhakikisha wanamuhudumia ili asiweze kuambukiza wengine, amesema, Mhe. Waziri Kindamba Mkuu wa Mkoa wa Songwe.
Afisa afya wa Mpakani Tunduma, Bi. Lulu Daudi Ngimba amesema wanapima wasafiri wote wanaovuka mpakani na wakimkutata mwenye dalili za Ebola anafanyiwa vipimo zaidi jujiridhisha.
Tuna weka umakini zaidi kwa wasafiri wanaotoka katika nchi zilizo athirika na Ebola, ili kuweka hali ya usalama kwa wananchi wa Mkoa wa Songwe na Taifa kwa ujumla, amesema, Bi. Lulu Ngimba.
Wakati huo huo, Mhe. Waziri Kindamba amewataka watanzania kuendelea kumuombea Afya njema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluh Hassan ili aweze kutekeleza majukumu ya kuleta maendeleo kwa Taifa.
MWISHO
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.