NIMEKUJA KUBORESHA MAZURI YOTE, RC MICHAEL.
SONGWE: Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Dkt. Francis Michael amesema amekuja kuboresha yale yote mazuri ambayo yamefanyika na watangulizi wake.
Mhe. Dkt. Francis Michael amesema hayo leo Machi 3 wakati akiongea na watumishi wa Ofisi ya Mkoa kwa lengo la kufamiana na kuweka mikakati ya kazi ili kufikia lengo la Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuwaletea maendeleo wananchi wa Songwe.
Mkuu wa Mkoa, Mhe. Dkt. Francis Michael amesema mikakati yote iliyowekwa ya maendeleo kwa wananchi wa Songwe itaendelezwa kwa kushirikiana na watumishi pamoja na wananchi.
"Katibu Tawala wa Mkoa ondoa hofu sitabadilisha jambo zuri ambalo mmelifanya nitajifunza mengi kutoka kwenu naomba ushirikiano wenu tutaboresha mikakati yote iliyofanyika na mtangulizi wangu" Mhe. Dkt. Francis Michael.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Bi. Happiness Seneda amesema watumishi wote wa Songwe wako tayari kutoa ushirikiano na kutekeleza maelekezo yote yatakayotolewa na Mkuu wa Mkoa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba, Mhe. Methew Chikoti akiongea kwa niaba ya Madiwani wa Mkoa wa Songwe amempongeza Mkuu wa Mkoa, Mhe. Dkt. Francis Michael kwa kuaminiwa na Rais wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuiongoza Songwe na kuhaidi kutoa ushirikiano wa kutosha.
Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Mhe. Solomon Itunda amesema watahakikisha wanaboresha ushirikiano na kuimarisha ili waweze kuleta maendeleo kwa wananchi.
Wakati huo huo, Mhe. Dkt. Francis Michael amemshukuru Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kuja kufanya kazi Songwe.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.