NJIA NNE KUTOKA TUNDUMA HADI MBEYA YANUKIA.
SONGWE: Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Waziri Kindamba amewapokea wakandarasi kutoka makampuni mbalimbali ambao wamekuja kuangalia Barabara ya TANZAM kutoka Tunduma-Mbeya kuona namna wanavyoweza kuanza kazi ya ujenzi wa Barabara ya njia nne (4) kutoka Tunduma hadi Mbeya.
Mhe. Waziri Kindamba amemshukuru Rais wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa moyo wake wa dhati wa kutatua changamoto ya foleni ya Malori katika Mkoa wa Songwe.
Pia, Mkuu wa Mkoa, Mhe. Waziri Kindamba amesema Mkoa wa Songwe ndio lango la SADC na ni kioo kwa wageni wanaoingia nchini, hivyo wageni watakapokutana na miundombinu bora inaleta sifa nzuri kwa Serikali ya Tanzania.
Aidha, Mhe. Waziri Kindamba ametoa wito kwa wananchi wa Songwe kuchangamkia fursa za kiuchumi pindi ujenzi utakapoanza.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.