Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli leo amezindua barabara yenye kiwango cha lami ya Tunduma-Sumbawanga yenye urefu wa Kilomita 223.2.
Rais Dkt Magufuli amefanya uzinduzi huo katika eneo la Laela Wilaya ya Sumbawanga na kuwasihi wananchi na viongozi wa vijiji jirani na barabara kutuza miundombinu ya barabara hiyo ambayo ina thamani ya shilingi bilioni 554.
Amesema wananchi hao wanatakiwa kuitumia barabara hiyo katika kujiletea maendeleo kwa kufanya biashara ndogondogo kwa watumiaji wa barabara hiyo pia kuitumia kusafirisha mazao katika masoko ya ndani na nje ya nchi.
Rais Dkt Magufuli amewapongeza watumishi wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mikoa ya Songwe, Rukwa na Katavi kwa kusimamia ujenzi wa barabara hiyo huku akiwataka kuendelea kusimamia miradi mingine ya barabara kwa kuzingatia gharama halisi na kubana matumizi.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.