Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Zambia Edgar Chagwa Lungu wamekutana leo na kuzindua kituo cha huduma za pamoja cha Tunduma-Nakonde.
Uzinduzi wa kituo hicho umefanyika katika eneo la Tunduma kwa upande wa Tanzania na kisha Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Zambia Edgar Chagwa Lungu waliekea kuzindua kituo hicho eneo la Nakonde upande wa Zambia.
Rais Dkt John Pombe Magufuli ameipongeza wizara ya Fedha kwa uamuzi wa kujenga kituo hicho kwakuwa Kituo hicho kitarahisisha shughuli za biashara huku akiwaasa maafisa wa forodha kusimamia weledi katika kuhudumia kituo hicho.
Aidha Rais Dkt John Pombe Magufuli amewataka wananchi na watumiaji wa kituo hicho kukitunza na kuwa mstari wa mbele kuwafichua watu wenye nia ovu ya kutaka kuhujumu miundombinu ya kituo hicho.
Naye Rais wa Zambia Edgar Chagwa Lungu amesema kituo cha Huduma za Pamoja cha Nankonde-Tunduma hupitisha zaidi ya mizigo 600 kwa siku na hivyo kurahisisha biashara kutoka Dar es Salaam hadi katika ushoroba wa kanda ya kusini mwa Afrika.
Rais Edgar Lungu amesema baada ya kuboreshwa kwa kituo hicho upitishaji wa mizigo umerahisishwa na kupunguza muda ambao watu walikua wanakaa mpakani kutoka siku 4 za awali hadi kufikia siku moja.
Rais Edgar Lungu amezishukuru serikali zote mbili kwa kuchukua hatua hiyo ambayo itawasaidia wafanyabiashara hususani wafanyabiashara wadogo.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.