RAIS SAMIA ARIDHIA WANANCHI WA NKANKA KUBAKI KWENYE HIFADHI.
ILEJE: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameridhia wananchi wapatao 3,000 wanaoishi katika hifadhi ya msitu wa Ileje Renger iliyopo kitongoji cha Nkanka Kijiji cha Itumba wilayani Ileje kuendelea kubaki kwa kuhakikisha wanatunza Mazingira wakati Serikali inaandaa utaratibu wa kuweka mipaka rasmi ya kitongoji hicho.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa kamati ya mawaziri wa kisekta inayoshughulikia migogoro ya Ardhi, Mhe. Dkt. Angelina Mabula ambaye ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakati wakiongea na wananchi wa kitongoji cha Nkanka Oktoba 24.
Dkt. Angelina Mabula ametoa miezi 2 kwa watalamu kuhakikisha wanatambua mipaka halisi ya kitongoji cha Nkanka ili wananchi wajue ni wapi wanaishia.
"Baada ya mipaka kuwekwa hatutarajii kuona mwananchi anaingia kwenye eneo la hifadhi, ukifanya hivyo ni kukiuka makubaliano na utachukuliwa hatua za kisheria" Dkt. Angelina Mabula.
Pia, Waziri wa Ardhi, Mhe. Dkt. Angelina Mabula ametoa wito kwa wananchi wa kitongoji cha Nkanka kuepuka kugawa Ardhi hovyo kwa wageni bila utaratibu, kwani Serikali haijafungukia milango kwa wageni kuvamia eneo ili ila wataingia kwa kufuata utaratibu.
Mhe. Dkt. Mabula amewataka watalamu kwa kushirikiana na wananchi wanapokwenda kupanga mpango bora wa matumizi ya Ardhi waweze kuzingatia sehemu ya huduma za jamii, Kilimo, mifugo pamoja na akiba kwa maendeleo ya Nkanka kwa miaka ijayo kutokana na eneo lao haliwezi kuongezwa.
Agnes Nyondo mwananchi wa kitongoji cha Nkanka amesema baada baadhi ya viongozi kuwaambia wahame wamejikuta wanashindwa kufanya mambo ya maendeleo, kama kujenga kulima kwani wamekuwa wakiishi kwa hofu, lakini tunamshukuru sana Rais wetu Mama Samia kwa uhamuzi wake wa sisi kuendelea kubaki hapa.
Ephraim Kayinga mkazi wa kitongoji cha Nkanka amewaomba mawaziri kuwafikishia salama kwa Rais Samia kwa uamuzi wake wa kuwabakiza kwani wao wamezaliwa Nkanka na maisha yao yoote yamekuwa hapa.
MWISHO
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.