Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila amewataka wadau wanaofanya shughuli za Lishe Mkoa wa Songwe kuangalia namna ya ufanya utafiti juu ya sababu halisi za Udumavu kwa Mikoa inayozalisha vyakula vingi kama Mkoa wa Songwe.
Kafulila ameyasema hayo alipokutana na wadau na taasisi zinazo jishughulisha na Afua za Lishe kwa Mkoa wa Songwe huku akieleza Kuwa Mkoa wa Songwe ni moja ya mikoa yenye vyakula vingi nchini hivyo ni vema kufanyike tafiti za sababu zipi hasa zinapelekea kuwa na asilimia kubwa ya udumavu.
“Wastani wa udumavu kitaifa ni asilia 32 lakini Mkoa wa Songwe tuna wastani wa 43 wakati huohuo sisi ni watatu kitaifa kwa kuzalisha chakula sasa hapo inabidi tafiti zifanyike zije na majibu ya uhakika kwanini tuna chakula kingi lakini bado kuna udumavu.”, amesema Kafulila.
Ameongeza kwa kuwapongeza wadau wote wanao shirikiana na serikali katika masuala ya Lishe kwakuwa ni kipaumbele cha Taifa kupambana na udumavu ambao ni janga kwakuwa huathiri ubongo wa binadamu.
Aidha Kafulila amewataka wadau na taasisi hizo kuhakikisha kuwa juhudi na shughuli mbalimbali wanazo fanya zinaleta mabadiliko katika kupunguza hali ya udumavu kwa Mkoa wa Songwe.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.