RAS SENEDA AWATAKA MAAFISA AFYA KUJA NA MIKAKATI YA KUSIMAMIA TAKA NGUMU.
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Bi. Happiness Seneda amewataka Maafisa Afya kuja na mikakati ya kitaalamu jinsi ya kusimamia taka ngumu ambazo zimekuwa changamoto kubwa sehemu za mjini haswa mji wa Tunduma.
Katibu Tawala, Bi. Happiness Seneda ametoa wito huo kwenye kikao kazi kilichofanyika Juni 1 kilichowakutanisha Maafisa Afya wote wa Mkoa kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
"Tunachangamoto kubwa ya usimamizi wa taka ngumu kwenye miji yetu ya Tunduma, Vwawa na Mlowo, unakuta taka ngumu zimekusanywa hovyo hovyo hali inayoweza kupelekea mlipuko wa magonjwa sasa lazima Maafisa Afya tuchukue hatua za kitaalamu" amesema Bi. Happiness Seneda.
Katibu Tawala wa Mkoa, Bi. Happiness Seneda amewataka Maafisa Afya kuwashauri vizuri viongozi kuanzia ngazi ya Kata, Halmashauri na Mkoa jinsi kuzisimamia taka ngumu kwenye jamii ili isiwe kero kwa wananchi.
Bi. Happiness Seneda amesema Mkoa wa Songwe unakua kwa kasi sana, hivyo ni lazima Maafisa Afya mje na mikakati ya kitaalamu ya jinsi ya kuzisimamia taka ngumu kwenye miji yetu ya sasa na ambayo inachipukia.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.