Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Bi. Happiness Seneda amelazimika kuvua viatu na kukanyaga maji akivuka mto Kisanda ili kufika kwenye mradi wa ujenzi wa madarasa na nyumba ya walimu katika Shule ya Msingi Rukwa iliyopo Kata ya Udinde Wilayani Songwe baada ya magari kushindwa kupita.
RAS Seneda ambaye aliambatana na sekretarieti ya mkoa, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe, CPA. Cecilia Kavishe na wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri ya Wikaya ya Songwe wamevuka katika mto huo leo Jumatatu Disemba 11, 2023 wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika Tarafa ya Kwimba Wilaya ya Songwe.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe ambaye anaongoza sekretarieti ya mkoa yupo Wilayani Songwe kwa ajili ya ziara ya siku tatu ya kufuatilia miradi ya maendeleo katika kata 18 na kuzungumza na watumishi wa Wilaya hiyo.
Katika ziara hiyo, Sekretarieti hiyo imekagua miradi mbalimbali ikiwemo ya elimu, miundombinu ya barabara pamoja na afya katika Tarafa ya Kwimba ambapo amewapongeza viongozi wa Halmashauri hiyo kwa utekelezaji wa miradi pamoja na kuwashauri namna nzuri ya kuweza kufanikisha miradi kwa wakati.
Baada ya ukaguzi wa miradi hiyo, Katibu Tawala huyo alikutana na kuzungumza na watumishi wa Tarafa ya Kwimba ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero zao
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.