RC ASHAURI VIWANDA VYA ALZETI KUFANYIWA MABORESHO YA KUCHAKATA MAZAO MENGINE YA MAFUTA.
SONGWE: Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba ametoa ushauri kwa wamiliki wote wa viwanda vya kusindika alzeti nchini kuweza kuvifanyia maboresho viwanda vyao ili viweze kusindika mafuta kwa kutumia mazao mengine jamii ya mafuta kama vile soya, karanga na michikichi.
Mkuu wa Mkoa wa ametoa ushauri huo alipofanya ziara katika kiwanda cha kusindika mafuta ya alzeti cha Majinja kilichopo wilayani Mbozi Julai 14 na kukuta moja ya changamoto ya kiwanda ni ukosefu wa malighafi kulingana na uwezo wa kiwanda.
Mkuu wa Mkoa amesema changamoto ya upatikanaji wa malighafi ni tatizo la nchi nzima kwani viwanda vilivyopo sasa vinauwezo wa kuzalisha tani milioni 2 kwa mwaka lakini mahitaji ya nchi ni tani milioni 1.5 lakini viwanda vilivyopo sasa vinazalisha zaidi ya tani laki 5 kwa mwaka na kufanya nchi kuagiza mafuta kutoka nje kwani uzalishaji uko chini.
“Kwa sasa viwanda vinahitaji kuzalisha tani milioni 1.4 lakini kutokana na ukosefu wa malighafi ya alzeti vinazalisha na kufanya viwanda vizalishe chini ya tani laki 6 kwa mwaka” Mhe. Omary Mgumba.
Kutokana na changamoto hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba ametoa wito kwa wamiliki wa viwanda vya kuchakata mafuta ya alzeti kubadili mfumo wa viwanda vyao ili viweze kuchakata mafuta ya soya pale ambapo wanakuwa wamekosa malighafi ya alzeti.
Mfano wananchi walio wengi wa Mkoa wa Songwe wananunua mafuta ya kupikia kutoka nchi ya Zambia ambayo yametengenezwa kwa soya, na sisi hapa tunalima soya kalanga hivyo ni wakati sasa wamiliki wa viwanda hivi kwenda kujifunza Zambia au kokote kule ili viwanda vianze kuchakata mafuta kwa mazao mbadala ya mafuta nasio kutegemea zao la alzeti tu.
Mkurugenzi wa kiwanda cha Majinja, Ndg. Alnanuswe Kabungo ameiomba Serikali kuhamasisha wakulima waweze kulima alzeti na kuichukua lazeti kama zao lao mbadala baada ya mazao waliyoyazoe ili Serikali iondokane nan a kuagiza mafuta kutoka nje ya nchi kwani kwa sasa ardhi ipo ya kutosha ni swala la wakulima wapewe elimu ili waweze kulima kwa ajili ya viwanda vyetu.
Aidha, Mkurugenzi wa Majinja, Bwn. Kabungo amesema ataufanyia kazi ushauri wa Mkuu wa Mkoa na ameishukuru Serikali ya Mkoa wa Songwe kwa kuweka mazingira rafiki ya kuwekeza ndani ya Songwe kwa kuweze kuimarisha ulinzi na usalama na wao kujisikia raha kusihi Songwe.
Akisoma taarifa ya kiwanda, Bwn. Agrey Kandonga amesema ifikapo Agosti 2022 kiwanda kitaanza uzalishaji wa tani eflu 12 za mafuta kwa mwaka sawa na lita laki 240,000 na mafuta yatakayozalishwa yatakuwa yanasafishwa mara mbili kwa ubora wa kimataifa.
Kiwanda cha kuchakata mafuta ya alzeti cha Majinja hadi kukamilika kwake kitagharimu kiasi cha fedha shilingi milioni 730 na kitakuwa msaada kwa wakulima wa Alzeti waliopo Mkoa wa Songwe.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.